SIMBA YAREJEA KAMBINI KUANZA KUJIWINDA NA KAGAME, NYOTA KADHAA KUYAKOSA MASHINDANO
Kikosi cha Simba kimeanza mazoezi leo ya kujiandaa na michuano ya KAGAME inayotarajiwa kuanza jijini Dar es Salaam Juni 28 2018.
Mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa White Sand uliopo uliopo jijini Dar es Salaam.
Simba wameanza mazoezi ya kwanza baada ya mapumziko mafupi ambayo walipewa kumalizika na sasa wamerejea tena kambini kuanza kujiwinda na mashindano hayo ya CRCAFA.
Kuelekea michuano ya KAGAME, inaelezwa baadhi ya nyota wa kikosi hicho ambacho ni bingwa wa msimu huu katika ligi watakosekana ili kuwapa mapumziko.
Jonas Mkude na Haruna Niyonzima ni baadhi ya wachezaji walioripotiwa kukosekana kwenye mashindano hayo.
Safari hii tusirudie makosa ya sportpesa cup
ReplyDeleteSafari hii tusirudie makosa ya sportpesa cup
ReplyDelete