June 14, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa Kamati Maalum wa kuivusha Yanga katika wakati huu wa mpito, Abassi Tarimba, amesema kuwa wamejipanga kufanya usajili wa kimyakimya.

Kupitia Radio EFM, Tarimba ameeleza kuwa inawabidi wafanye hivyo kwa nia na madhumuni ya kurejesha makali ya timu kama ilivyokuwa mwanzo baada ya kuyumba hivi sasa.

Tarimba amefunguka na kusema kumekuwa na baadhi ya klabu zimekuwa zikisubiri Yanga itaje wachezaji wa kusajili kisha zinaibuka na kuwanyakuwa, hivyo itawabidi waende kimyakimya kufanikisha usajili.

Yanga mpaka sasa imeshamalizana na mchezaji wake wa zamani Mrisho Ngassa pamoja na Mbenin Marcellin Koukpo ambaye inaelezwa ameshaini mkataba wa miaka miwili.

Mbali na wachezaji hao, Yanga imekuwa imeanza mazungumzo na mshamuliaji hatari wa Gor Mahia FC, Meddie Kagere ambaye ametaka kiasi cha milioni 180 pamoja mshahara wa kiasi cha milioni 11 kwa mwezi ili aweze kujiunga na mabingwa hao mara 27 wa Ligi Kuu Bara.

5 COMMENTS:

  1. Imekuwa imeanza????? Ni kilugha au?

    ReplyDelete
  2. Kagere mzuri ila umri wake unaleta shaka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ana miaka 33 inawezekana miaka 3 zaidi akawa kwenye ubora huu wa sasa na kipindi hicho atakuwa katumikia timu vizuri inatosha

      Delete
  3. KWELI KAGERE WATAMCHUKUA KWA GHARAMA NYINGI THEN ATAKUJA KUWA KAMA BONIFACE AMBANI AMBAYE ALING'AA MSIMU MMOJA PEKEE

    ReplyDelete
  4. Itabidi Sportpesa itafute mwakilishi mwingine Tanzania kwani inaweza kuwa ngumu kwa yeye kujigawa katika kutekeleza majukumu yake hivyo kuwepo kuwepo conlict of interest

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic