June 14, 2018


Salamu, naona wakati Umefika acha niseme kidogo, nasema kwa kuwa kila jambo Lina wakati wake na muda wake na Majira yake.

Najua mtauliza Kwanini Nasema sasa, JIBU ni jepesi tu ndio WAKATI Wangu wa Kusema sasa acha niseme.

1. Yanga itajengwa na wana Yanga Wenyewe, Najua Msingi wa Yanga ni wanachama , Mashabiki na Wapenzi na huu ndio Mtaji Mkubwa kuliko wote ambao Mungu ameitunuku Yanga, Uwepo wa Mamilioni ya Wananchi wanaoipenda Yanga (Comsumers) ndio chanzo cha kwanza kikuu cha Mapato, Ila Shetani Ameleta laana ya kutolijua Hili katika ufahamu wetu, Katika maisha ukishindwa kujitambua Ni sawa Na MFU , Yanga kwa Muda mrefu Imeshindwa kutumia mtaji wa RASILIMALI ya wanachama wake kama Mapato hii ni LAANA , na ndio mana kila njia tunayotumia Tumeshindwa, lazima ifike mahali tujiulize kwa nini Tumeshindwa kuifanya Yanga Ijitegemee, badala yake tumeifanya Yanga kumtegemea mtu, katika vitabu vitakatifu vya kwetu vimeandikwa "amelaaniwa Amtegemeae Mwanadamu, na kumfanya nguzo yake"
-Viongozi wetu ama kwa Makusudi au Kiburi wameshindwa kuliona hili kwa kuwa Wana maslahi yao binafsi au ni choyo ya kutaka kuonekana wao ndio Msaada pekee kwa Yanga, pasipo kutambua kuwa Yanga ilikuwepo kabla ya Wao kuzaliwa.

Wameshindwa kusimama IMARA kwa kuwaeleza Wanachama majukumu yao na wajibu wao kwa klabu HUENDA ni kwa sababu wanataka KURA za ndio kila uchaguzi, na wako wengine pasipo Aibu uku wakijua chanzo kikuu cha mapato ya Yanga ni Ada za kila Mwezi za wanachama Wanadiriki kuwalipia wanachama Hela za Kadi kwa Mwezi Mmoja tena Siku kadhaa Karibu na Uchaguzi, Huu ni UPUUZI , iweje Ushindwe kuhamasisha Wanachama kulipia kadi zao kila Mwezi Badala Yake Uwalipe wewe mwezi Mmoja wa Uchaguzi? Lazima tukushike "UCHAWI " kuwa wewe ndie MDUMAZA Maendeleo ya Yanga kwa Tamaa zako za Kutawala Yanga na SIO KUONGOZA , Mana Katika Hili wamekosa sifa ya Uongozi.

2. Yanga inahitaji Kiongozi Mwenye akili ya kutumia RASILIMALI watu (Wanachama) na kuigezua kuwa Mtaji wa Kuendesha Yanga, Yanga ya sasa Haiitaji Tajiri, inahitaji Mtu Mzalendo Mwenye Maono, Akili na Ujuzi wa Hali ya Juu ya Kuibadilisha Yanga kutumia RASILIMALI mfano Yanga ikiweza kuhamasisha watu milioni moja Kati ya milioni 45 tulionao, na tukiweza kupata wanachama milioni tunachopaswa ni kuwaomba waichangie Yanga Shilingi elfu moja tu kwa mwezi jambo ambalo litawawezesha kila mtu kuichangia Yanga hata wale wafanyabiashara ndogo ndogo ambao ndio wengi, ukiwa na mfumo huu utaweza kuvuna Shilingi bilioni moja kila mwezi kwa njia za kisasa zaidi mfano mifumo ya Atm za kibenki, mifumo ya Pesa kwa njia ya simu Mpesa, TigoPesa, airtekMoney, Tmoney na zingine.

Hili lingewezekana wakati ule ambao Yanga Inafanya vizuri tulipochukua Ubingwa Mara mbili na kumfunga simba mara mbili kwenye ligi, na kuchukua Ubingwa Wa FA na pia kuingia Robo Fainali, kama Viongozi hawa Walitaka hili lifanikiwe ule ndio ulikuwa Wakati Sahihi wa Kuomba wanachama na Wangechanga, NAJUA utauliza Kwanini Hatukufanya? JIBU rasmi nitawapa siku Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Wakithubutu kufungua Mdomo kujibu hili, ila itoshe kusema UCHOYO , UBINAFSI au KUTOJUA WAJIBU vilikuwa Pembeni ya ROHO zao, ila nitakuja siku kusema Ukweli katika hili. 

3. Yanga Inahitaji Mabadiliko ya Mfumo , na Muundo utakaoruhusu Mtu mwenye akili Kuongoza Yanga , katika Mfumo na Muundo wa Sasa Yanga inateseka mana Inatafuta Tajiri wa kuikwamua, ndugu zangu wana Yanga Mnisamehe kwa Maneno Haya Mazito "HAKUNAGA URAFIKI KATI YA TAJIRI NA MASIKINI" , ili tajiri aendelee kuwa tajiri lazima Ahakikishe watu Wanaomzunguka Wanakuwa Maskini kila siku ili WA MPIGIE MAGOTI , kasomeni Biblia au Kuran takatifu mtaona, Tubadili Mfumo na Muundo.

4. Yanga Inahitaji UWEKEZAJI na Sio Tajiri, Naomba mnielewe Yanga ni Taasisi na katika hili Yanga inahitaji Taasisi Nyingine katika Kufanya Biashara, mana Mfumo wa uchumi unategemeana Taasisi zinahitaji Yanga na Yanga inahitaji Taasisi, tunachokosea Yanga tunatafuta mtu afanye Biashara na Taasisi Hii katika Mahesabu Haiwezekani, hata katika Maisha, mana Yanga ni Taasisi Haifi, ila mtu Anakufa utake usitake, Sasa ili kujenga misingi Imara ili mtu akifa au kupata majanga Yanga isihadhirke Itafutwe taasisi Iingie kwenye Makubaliano ya Uwekezaji na Yanga , nakumbuka tulitaka Kujaribu hili na Mimi nilikuwa Muumini Mzuri na Nilipigania Mwenyekiti Aruhusiwe Kuwekeza kwa Nguvu Sana lakini Mzee Akili Mia na Genge Lake wakaweka Stop. 
-Katika Hili Mkumbuke kuna Masuala ya Mtaji (Capital) na Hisa (Shares) lazima Viongozi waliopo wakubali kutoa Elimu kwa Wanachama kujua Hivi Vitu na wakivijua Watavieleewa na Kuupokea Uwekezaji.

Hitimisho 
Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga Wanapenda Maendeleo na Wamechoka Kuumia Roho, Wanataka Furaha ya Miaka Ile, Wanachohitaji Ni Kuelimishwa , Kufundishwa na Kuelekezwa Namna Bora ya Kuinusuru Yanga hapa ilipo, Wajanja Wasitumie Mwanya wa "Dhiki " hii kufa Wanavyotaka, Lazima kuwepo na Utaratibu hata kama Tutachelewa Yanga ni Yetu Sote. 

Kupanga ni kuchagua, hakuna namna tuchague sasa

 Jerry C. Muro
 Lagos Nigeria
 14/06/2018

9 COMMENTS:

  1. Jerry wewe ni mwanachama wa Yanga, haya unayoyasema nenda kayasemee kwenye vikao halali vya chama ili mjadiliane na kukubaliana, hapa unapoyasemea sio mahala pake na ni kinyume na utaratibu.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Haya ni maneno mazuri lakini sio hapa kwenye magazeti sio mahali pake, kuna sehemu yake kiutaratibu, kikanuni na kisheria...kwani nchi inaamini katika uhuru wa maoni ili mradi hauvunji sheria....lakini useme katika majukwaa husika, bila kuchochea na kuvuruga amani ya nchi. Narudia ni maoni mazuri lakini sio mahali pake. Yanga ina vikao vyake kikatiba huko ndipo ambapo maoni yanapelekwa

    ReplyDelete
  4. JERY MURO ANAMAWAZO MEMA LAKINI AMEYATOA KWA MAJUNGU KWASABABU ANGEWEZA KUSHAURI UONGOZI BILA KUANDIKA MAGAZETINI, INAONEKANA KUNAKUNDI FULANI LINAMTUMIA HUYU,, MURO NA AKILIMALI WANATUMIKA NA MAKUNDI AMBAYO KILA MOJA LINAMASLAHI NDANI YA YANGA.

    ReplyDelete
  5. Jerry huna jipya, wenzio walishayaona hayo na wakajaribu lakini hawakufika popote. Mfano mzuri ni wewe ulichangisha pesa kwa ajiri ya Manara, hebu twambie ulipata milioni ngapi!? Kama wewe hukuweza kuchangisha hata milioni moja, iweje ufikirie wenzio kuchangisha bilioni kila mwezi!? Kwamba viongozi wote wa Yanga, Simba, nk ni wajinga ila we ndo mwelevu!? Jerry unatumika, na wanaokutumia kwa njaa zako tunawajua. Ukieendelea na huu ujinga tutakuumbua!? Manji unayemponda leo ndiye aliyekuwa anakulisha wewe na familia yako. Leo ameacha kukupa hela za bure, unaanza kumchafua mtandaoni kisa wapinzani wanakupa vimia miambili vya kula na kunywa!? Acha njaa, na ukienda extreme utaumia!! Acha ujinga huu, wewe huna tofauti na Akili Mali, mnatumika kwa maslahi ya wachache kwa njaa zenu.

    ReplyDelete
  6. Mawazo ni mazuri na yanajulikana na kila MTU mwerevu.

    Kwanza yy mwenyewe karukia gari kwa mbele. Anasema yote yanawezekana Yanga ilipochukua ubingwa Mara mbili mfululizo na kombe la FA.

    Asiwe mnafiki aseme pia Yanga ile ilifikishwa pale na nani?

    Kama anajua ili timu ifanikiwe inatakiwa iwe na ushindi endelevu nani ? Atufikishe hapo?

    Jerry asijisahaulishe, na waandishi na watangazaji muwe na kumbukumbu, Jerry huyu huyu akiwa kiongozi Yanga.

    Aliulizwa maendeleo ya Yanga chini ya Manji alisema Manji ameisha onesha njia ni jukumu la wanayanga kusonga mbele.

    Leo yupo nje anasema Mwenyekiti na makamu walikuwa kikwazo. Shame shame

    ReplyDelete
  7. Mawazo ni mazuri na yanajulikana na kila MTU mwerevu.

    Kwanza yy mwenyewe karukia gari kwa mbele. Anasema yote yanawezekana Yanga ilipochukua ubingwa Mara mbili mfululizo na kombe la FA.

    Asiwe mnafiki aseme pia Yanga ile ilifikishwa pale na nani?

    Kama anajua ili timu ifanikiwe inatakiwa iwe na ushindi endelevu nani ? Atufikishe hapo?

    Jerry asijisahaulishe, na waandishi na watangazaji muwe na kumbukumbu, Jerry huyu huyu akiwa kiongozi Yanga.

    Aliulizwa maendeleo ya Yanga chini ya Manji alisema Manji ameisha onesha njia ni jukumu la wanayanga kusonga mbele.

    Leo yupo nje anasema Mwenyekiti na makamu walikuwa kikwazo. Shame shame

    ReplyDelete
  8. Ametumwa huyo siyo bure,yanga inamuitaji manji awekeze na ndio ilikuwa nia yake tangu mwanzo,miaka yote ulikuwa yanga kwa mini nakupigia debe kama unavyofanya sasa,endelea na maisha yako tuachie yanga yetu,na kwa nini hukuja kwenye mkutano juzi,yanga ni kubwa kuliko wewe,na waliokutuma washindwe kabisa.

    ReplyDelete
  9. Muro kaweka chungu hapa na moto kutoka chunguni mita mis. Ili chakula kuiva weka chungu juu ya moto bwana usiwe unaweseka tu au mtaambulia patupu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic