June 1, 2018


Baada ya kumtangaza Kocha Hans van der Pluijm kuwa mrithi wa Mromania, Aristica Cioba, uongozi wa Azam FC kupitia Ofisa wake wa Habari, Jaffer Idd Maganga, umesema kuwa utalipua bomu Jumatatu.

Awali Azam ilitegemewa kuwatambulisha wachezaji iliowasajili jana katika mkutano iliotisha na Waandishi wa Habari, lakini badala yake akatangazwa Kocha Pluijm pekee.

Maganga ameeleza kuwa kuwa sasa itabidi waitishe kikao kingine na Waandishi wa Habari ili kuwatambulisha wachezaji hao siku ya Jumatatu huku akisema litakuwa bomu kwa wapinzani wao.

Tetesi zilizo chini ya kapeti inaelezwa Azam wameshamalizana na beki wa kulia wa Yanga, Juma Abdul huku pia baadhi ya wachezaji wengine ikiwemo Andrew Vincent naye akiwindwa na matajiri hao.

Tayari Azam imeshanyakua Mzimbambwe aliyekuwa akiichezea Yanga, Donald Ngoma ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic