July 13, 2018


Na George Mganga

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni nchini kutoka saba mpaka 10, Kocha wa klabu ya Simba, Masoud Djuma, amesema ni jambo jema kwao.

Djuma ambaye amekuwa akikiongoza kikosi cha Simba tangu kuondoka kwa Pierre Lechantre ambaye alichukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog, kisha kusepa zakwe baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika, amesema ni faida kwao kutokana na kukabiliwa na mashindano ya kimataifa.

Akizungumza mara baada ya mazoezi ya jana kumalizika kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Djuma ameweka wazi kuwa ni faida kwa Simba kwasababu watakuwa wanaiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Kuongezwa kwa wageni kumemfanya kocha huyo kuwa na imani ya kukijenga kikosi cha Simba vizuri kuelekea mashindano hayo makubwa kwa Afrika ambapo amesema wana ahadi kutoka kwa Rais Magufuli kuwa wanapaswa kulitwaa taji hilo.

Ikumbukwe wakati Simba wanakibidhiwa kombe la ligi na Rais Magufuli kwenye uwanja wa taifa, Dar es Salaam, aliwataka wawe wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kulibeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Uamuzi wa TFF kuongeza idadi hiyo inawapa nafasi Simba ya kukipanua zaidi kikosi chao ambapo wamekuwa wakihusishwa pia kumsajili kiungo wa Gor Mahia FC, Francis Kahata ili kuongeza nguvu katika safu ya kiungo.

Aidha, Simba ipo kwenye mazungumzo na kiungo Mcongo, Fabrice Kakule ambaye amewasili takribani ana wiki sasa kufanya majaribio na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 kutoka Kiyovu SC ya Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic