July 9, 2018


Uongozi wa klabu ya Alliance kutoka Mwanza umewalalamikia Singida United kwa madai ya kumchukua mchezaji wao Athanas Adam.

Taarifa kutoka Mwanza zinaeleza kuwa uongozi wa juu wa Alliance umefikia hatua hiyo za kuwatumia lawama kali Singida kumchukua mchezaji huyo kinyemelea bila kufuata taratibu.

Kwa mujibu wa Radio One, Alliance wameeleza kuwa Singida walipaswa kuongea nao kuliko kumnyatia mchezaji huyo kwa mlango wa uani na mwisho wake wakamchukua bila kufuata taratibu stahiki.

Aidha, uongozi wa Alliance umefunguka na kusema Singida wamekuwa na tabia hiyo wakieleza kuwa si mara ya kwanza kuwachukulia wachezaji wao.

Lakini Mkurungenzi wa Singida United, Festo Sanga alipotafutwa kujibu lawama hizo alipinga na kusema hawana mchezaji waliyemtabulisha anayejulikana kwa jina hilo.

Sanga amejibu na kueleza si kweli na lawama wanazopewa hazina uhakika kwani hawajatambulisha mchezaji anayeitwa Athanas.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV