Beki Bryan Melisse wa F91 Dudelange amegeuka gumzo katika soka duniani kote kutokana na rafu mbaya aliyocheza.
Melisse alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumrukia beki wa Videoton, Mate Patkai kwa mfumo wa Kung Fu. Mechi hiyo ilikuwa katika timu ya Luxembourg dhidi ya inayotokea nchini.
Ilionekana F91 Dudelange kutoka Luxembourg ilikuwa inatolewa baada ya kuwa imefungwa mabao 2-1 na mwisho kwa ujumla ingekuwa ni 3-2 na dakika zilikuwa zinayoyoma.
Hali hiyo ilimchanganya beki huyo raia wa Ufaransa ambaye aliamua kuruka na kumkanyaga mchezaji wa timu pinzani kwa mfumo wa Kung Fu.
0 COMMENTS:
Post a Comment