Kampuni ya Multichoice Tanzania jioni ya leo imezindua msimu mpya wa Kipindi cha Harusi yetu ambacho hurushwa katik king’amuzi chake kwenye chanel namba 160.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi, alisema baada ya kipindi hicho kuonekana kuwa na mashabiki wengi ambao walikuwa wakikifuatilia kwa ukaribu zaidi wamelazimika kuzindua sehemu hiyo ya tatu ili waweze kuwaonyesha mauzui bora zaidi.
Pamoja na uzinduzi huo pia Kambogi ameeleza kuwa kwa muda wote sasa watakuwa wakiendelea kushirikiana kwa karibu zaidi na waigizaji wote nchini ili waweze kuitumia chanel hiyo kutangaza kazi zao.
Kwakuanza sasa wana vipindi kibao ambavyo hurusha tamthiria mbalimbali na filamu za hapa nchini na pia kuna tamthilia nzuri za wasanii wa kitanzania kama vile Uber na mwantumu ambazo kwa pamoja zinafanya vyema.
0 COMMENTS:
Post a Comment