July 20, 2018Wakati ukiwa umesalia mwezi mmoja pekee huu wa saba kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Bara 2018/19, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, ametoa masharti kadhaa kwa klabu zinazosajili wachezaji wa kigeni.

Kwa mujibu wa Radio One, Wambura amesema kwa kila timu inayotaka kusajili mchezaji wa kigeni ni lazima ihakikishe ana ubora wa kutosha na si ilimradi awe anatoka nje ya Tanzania.

Mbali na ubora, Wambura ameeleza mchezaji yoyote wa kigeni anapaswa kucheza na si kukaa benchi ili kuonesha kweli kuwa yeye ni wa kimataifa halisi na si wale ambao wamekuwa wakiletwa kisha wanashindwa kucheza.

Vilevile Wambura amezitaka klabu zote endapo zinasajili wachezaji wa kigeni ziwe na uwezo wa kuwalipa mishahara yao vilivyo na isije ikatokea wanadai kwa maana watachukua hatua kwa wahusika.

"Tunataka klabu ikishasajili mchezaji wa kigeni ni lazima kwanza iwe na uwezo wa kumlipa stahiki zake zote ikiwemo mshahara, hatutaki kusika anadai, pia tunataka mchezaji huyo awe na uwezo unaoashiria kuwa ni wa kimataifa na si wa kukaa benchi" alisema Wambura.


4 COMMENTS:

 1. Hivyo suala la kocha wa timu ya Taifa limeishia wapi au always next time?
  Rundo la makocha waliojaa duniani vipi tunashindwa kuwa na kocha wa Taifa? Kinachokera zaidi ukimya wote huu kana kwamba kuna mikakati ya kimya kimya ya kutafuta kocha wa maana lakini mwishowe akija kutangazwa huwa kocha asiekuwa na ubora wowote ule. Nafasi ya kocha wa timu ya Taifa ni bora wadau wahusika wakamleta kocha mwenye viwango tosha si bora kocha tu. Makocha wengi walioletwa au walioajiriwa kuifundisha taifa stars kwa miaka ya hivi karibuni walikuwa ni makocha wa majaribio sio makocha wa mafanikio. Tunajua wakati wa TFF YA Malinzi makocha waliajiriwa kikamesheni zaidi yaani wahusika walijali kutengeneza kitu zaidi ndani ya mkataba wa kocha kuliko ubora wa kocha. Tunawaomba TFF kuweka mjadala wa wazi kuhusiana na suala la kocha wa timu ya Taifa ili kuindoa sintofahamu inayoendelea. Sio kocha kwakuwa anatoka brazili basi atakuwa kocha hapana inatakiwa lazima awe na takwimu bora za mafinikio. Si kocha kwakuwa anatoka ufaransa basi atakuwa kocha hapana inatakiwa lazima awe na takwimu za mafanikio. Wamekuja makocha wengi kama akina Maximo kutoka Brazil. Halafu akaja yule MdenDenmark polusen, Halafu akaja yule Mholanzi wa hovyo wa Malinzi, halafu hawa akina charles Bonafasi, Mayanga, Morocco na kumalizia na akina Ame Ninje. Sasa ukiangalia wasifa wa makocha hawa hakika CV zao za mafanikio yao katika ngazi ya timu ya taifa kwa kweli ilikuwa ni kupoteza muda na rasilimali za Taifa, kwani kulikuwa hakuna kocha hata moja aliekuwa na sifa stahiki. Watanzania tunatatizo la kutojifunza kutokana na makosa yetu ya nyuma. Na vile vile tunakosa viongozi wa soka mashupavu wanaowaza makubwa na kudiriki kuyatendea kazi. Katika mpira hakuna siasa bali kuna matokeo na ni matokeo yatakayowaeleza watu kuliko mdomo lakini kwa sasa timu yetu ya Taifa kuna siasa zaidi kuliko matukio chanya. Mimi licha ya kelele za watu yakuwa Simba haikai na makocha lakini walahi wanawaheshimu sana Simba kwani pale Simba inaonesha sasa wana viongozi wanaowaza makubwa na kudiriki kuyatendea kazi hayo makubwa wanayoyawaza kwani ilikuwa kama vile unasoam kitabuni kusikia simba iliajiri kocha alieipa moja ya timu vigogo Africa ubingwa wa Africa? Hata Almasry walishtushwa na kuingia mchecheto baada ya kukutana na kocha yule. Kwakweli siamini kama simba inauwezo huo mkubwa wa kifedha ila ninachokiamini wana viongozi wenye ujasiri wa kudream BIG na kujaribu kutekeleza kwa vitendo. Ujasiri kama unaoneshwa na kiongozi wetu mkuu wa nchi muheshimiwa Magufuli. Na sio mbali sana Simba watafanikiwa kupata kile wanachotarajia kwani katika hali ya kawaida ungeweza kusema Masoudi Djuma anatosha kuwa kocha mkuu pale Simba. Lakini uwepo wa uthubutu wa ndani ya viongozi wa simba wa kuona timu yao inafika mbali ziadi ya macho ya kawaida ya mtanzania wa kawaida wameamua kumleta kocha aliepata majaribu mengi zaidi katika kazi kuliko Masoud na huko ndiko kuwaza big na kuwa na ujasiri wa kuifanyia kazi kwa vitendo yale makubwa unayoyawaza hongereni sana Simba naimani siku si mbali mtaandika historia katika nchi hii kwenye ulimwengu wa Soka ila TFF hawana haja ya kuona aibu kufuata nyayo zenu kwani huu ni wakati wa Magufuli ni wakati wa mageuzi ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali na bora kuwepo na kauli mbiu yakwamba asiekuwa tayari na harakati za mageuzi ya kimaendeleo kwa kwa sasa Tanzania basi mageuzi yatumike kumgeuza yeye na kumtafuta alietayari kukabiliana na changamoto kikamilifu.

  ReplyDelete
 2. Bila kuegemea kweny neno simba huuzi. Kwann usiseme Bodi ya ligi yaipga mkwara singida?au yanga? Kwan wao hawasajiri awo nyota wa kigeni????
  Ndo ujifunze sasa kuwa mpira ni pesa na kutengeneza brand yacclub sio mchezo.
  Endelea na mtazamo wako kuvipublish vizee vipinga maendeleo soka la bongo

  ReplyDelete
 3. Bodi muache ubabaishaji na kutoa maelekezo kwa marefa kupendelwa timu na mipango kandamizi kwa vilabu,ratiba mbovu bila kujali kalenda zingine,udhamini usiokidhi kwa timu

  ReplyDelete
 4. pointi ni moja tu ya mshahara hizo nyingine ni hamasa tu

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV