BREAKING: LIVERPOOL SI MCHEZO, YAMNASA BECKER, AMWAGA WINO WA MIAKA SITA ANFIELD
Klabu ya Liverpool imefanikiwa kumsajili kipa aliyekuwa akiichezea AS Roma kwa kuingia naye mkataba wa miaka 6.
Liverpool wamefikia makubaliano na mlinda mlango huyo ambaye alikuwa anawania na baadhi ya klabu zingine England ambapo dau la pauni milioni 67 limeweza kumuondoa Roma.
Usajili huo umefanyika ili kuboresha nafasi ya mlinda mlango baada ya Loris Karius kuonekana kuwa na mapungufu kadhaa yaliyosababisha bodi ifanye harakati za kusaka kipa mwingine.
Ujio wa Becker unawapa wakati mgumu Simon Mignolet na Karius kutokana na ubora mkubwa wa Becker ambaye ni kipa namba moja wa timu ya taifa ya Brazil.
Yap chama la wana
ReplyDelete