July 12, 2018



Hatimaye kiungo  Feisal Salum Abdalah “Fei Toto” ametambulishwa rasmi na uongozi wa klabu ya Yanga.

Fei Toto kutoka JKU amejiunga na Yanga akisaini mkataba wa miaka mitatu ikiwa ni saa chache baada ya kutangazwa amejiunga na Singida United.


Singida United kupitia Mkurugenzi wao, Festo Sanga, leo mchana walimtangaza Fei Toto kuwa amejiunga nao wakionyesha picha wakati anasaini na kukabidhiwa jezi za Singida United.

Lakini leo, Yanga imemtangaza rasmi kutua Jangwani huku ikielezwa mkataba wa Singida United ulikuwa na matatizo.

Baadaye wakasambaza video zikimuonyesha akieleza alivyojiunga na Singida United lakini hivi punde atatambulishwa Yanga.

Pamoja na Fei Toto alionekana akizungumzia kwenye video kueleza alivyotua Singida United na ataitumikia msimu ujao.

Pamoja na kumsaini Fei Toto, Yanga pia imsajili Jaffar Kibaya kutoka Majimaji kwa mkataba wa miaka miwili.



15 COMMENTS:

  1. Sasa mbona hawasemi wanasaini kimya kimya kuogopa wataporwa. Na wao huyu si alishasaini Singida mbona wanapora? mkuki kwa nguruwe

    ReplyDelete
  2. Jafary Kibaya alikuwa Kagera na amesaini Mtibwa

    ReplyDelete
  3. Sio mara ya kwanza kuna aliyesaini Simba mwaka jana halafu wakampora...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na Buswita mwaka jana alisaini Simba kwanza na kisha Yanga pia.Buswita akadai shetani alimpitia.Huyo Toto itakuwa dawa ya Yanga imemuingia.

      Delete
    2. shetani alimpitia ??? wachezaji wa bongo hatari sana.

      Delete
  4. Mbona hili picha silielewi elewi duuuh! Mpira kweli fitna

    ReplyDelete
  5. Usajili una njia zake, ukiziuata siku zote utakuwa salama.
    Ongea na mchezaji, kisha klabu yake.

    Ukidharau umekwisha, Rage anakumbuka Mbuyi Twite .

    Buswita ,Simba walidharau mkataba Wa mwezi mmoja mbao.ambao Yanga waliuheshimu na kuununua.

    ReplyDelete
  6. Usajili una njia zake, ukiziuata siku zote utakuwa salama.
    Ongea na mchezaji, kisha klabu yake.

    Ukidharau umekwisha, Rage anakumbuka Mbuyi Twite .

    Buswita ,Simba walidharau mkataba Wa mwezi mmoja mbao.ambao Yanga waliuheshimu na kuununua.

    ReplyDelete
  7. Tunalo tatizo nchini kwetu. Wapo watu matapeli wanaodanganya na kuwapora pesa watu kwa udanganyifu na njia za simu hawa wanaporipotiwa jeshi la polisi huwasaka na kukamatwa na kuchukuliwa hatua. Inakuwaje mchezaji waziwazi anatapeli timu halafu ajabu badala ya watu kukilani kitendo cha kitapeli ajabu watu wanashabikia na kuhalalisha kitendo hicho cha ovyo kabisa. Hivi umesikia wapi nje huko mchezaji kusaini na kuchukua pesa za usajili timu mbili msimu mmoja? Jamani tunajitia ujinga tuache utapeli huu hautupi heshima.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Singida wamshitaki huyo mchezaji kwa utapeli

      Delete
    2. Wampeleke Mahakamani tu itakuwa fundisho kwa wengine kutokuwa na tamaa ya kutapeli

      Delete
  8. Nijaffary Mohammed toka Majimaji na sio Jaffary kibaya huyo alijua kagera amesain mtibwa

    ReplyDelete
  9. Yaleyale ya Mbuyu Twita lala hela ya Simba asubuhi na jioni kuchukukuliwa na Yanga, pale yanga ilipokuwa yanga kweli sio tanga ya madeni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic