July 12, 2018


Mashabiki wamejazana katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, tayari wakisubiri utambulisho wakiungo  Feisal Salum Abdalah “Fei Toto”.


Wakati Toto alikuwa ametangazwa kuwa ametua Singida United, lakini Yanga jioni hii wanatarajia kumtambulisha.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi makao makuu hapo Jangwani na Twiga.


Singida United kupitia Mkurugenzi wao, Festo Sanga, leo mchana walimtangaza Fei Toto kuwa amejiunga nao wakionyesha picha wakati anasaini na kukabidhiwa jezi za Singida United.

Baadaye wakasambaza video zikimuonyesha akieleza alivyojiunga na Singida United lakini hivi punde atatambulishwa Yanga.

2 COMMENTS:

  1. Ignorance ya wachezaji wetu ndiyo inatudhihirisha hapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni ignorance ya mwandishi tu akijitafutia umaarufu wa habari. Hakuna ukweli na anachokiandika.

      Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV