KIONGOZI YANGA AAHIDI KIKOSI KUFANYA MAAJABU HAYA LEO VS GOR MAHIA AELEZA KITAKACHOWAPA UGUMU
Mwenyekiti wa Matawi katika klabu ya Yanga, Bakili Makele, ametamba kuwa kikosi chao kuelekea mechi dhidi ya Gor Mahia ya mchezo wa Kombe la Shirikisho kitaleta maajabu.
Makele ambaye amekuwa akiviteka vyombo vya habari siku za hivi karibuni kutokana na matamko yake juu ya TFF, amesema maandalizi ya mchezo huo yako vizuri na timu ipo tayari kwa mchezo.
Mwenyekiti huyo ana imani matumaini ya Yanga kufanya vizuri yapo huku akisema changamoto moja inayowakabili ni kuwakosa baadhi ya wachezaji.
Mabeki Hassan Kessy na Kelvin Yondani, amewataja kama wachezaji ambao wanaweza kuleta pengo kutokana na kubakia Dar es Salaam akieleza kuwa sababu hawakuwa kwenye ratiba ya mazoezi ya Kocha Mwinyi Zahera.
Mchezo huo wa mkondo wa kwanza unatarajiwa kupigwa majira ya jioni jijini Nairobi ambapo Yanga inapaswa kupata matokeo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele.
KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANYA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!
ReplyDeleteManeno hayaoani na uhalisia Wa timu.mnafanya mchezo na maisha ya uhai Wa club ya Yanga.mumekosa sofa.acheni pwapwapwa .Maneno hayachezi Moira.uongozi unamaneno mengiiii tangu mwanzoni mwa msimu vipi Yondani ,na Zahara,Messy Ngasa ,Kaseke ns mkongo wawe inje ya mechi hii muhimu? Siasa kwenye mambo muhimu ?poleni.
ReplyDelete