July 22, 2018


Uongozi wa klabu ya Coastal Union iliyorejea Ligi Kuu Bara umefunguka kuhusiana na Msanii Ali Saleh Kiba juu ya kumsaini kwa ajili ya kuichezea timu hiyo.

Siku takribani mbili zilizopita taarifa zileleza kuwa Coastal wameanza mazungumzo na Kiba kwa ajili ya kuingia naye mkataba ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji.

Taarifa kutoka ndani ya Coastal Union zinasema uongozi wa klabu hiyo umeeleza kuwa Kiba aliwafuata akiomba aichezee timu hiyo kwani anaipenda na anaupenda mpira.

Baada ya Kiba kuwafuata, Coastal wamesema wameamua kusikiliza ombi lake na sasa wapo kwenye mazungumzo ya kumalizana naye na ikiwezekana anaweza akawa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao.

Tetesi za Kiba zimetekea vichwa vingi vya habari katika vyombo vya habari kutokana na kuzoeleka kwake zaidi kwenye tasnia ya muziki tofauti na mpira ambapo amekuwa akicheza kwa kujifurahisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic