July 22, 2018


Na George Mganga

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, ametoa ushauri kwa wekundu wa Msimbazi kuhusiana na usajili wa timu hiyo.

Kwa mujibu wa Radio One, Katika kipindi hiki cha usajili ambao umebakiza siku tano kufungwa, Rage amewashauri mabosi wa Simba kumwachia Kocha majukumu yote ya kupendekeza wachezaji.

Kauli hiyo imekuja kutokana na kasumba ya viongozi wengi wa soka la Tanzania kufanya usajili wao badala ya makocha kupewa mamlaka,.

Rage ameeleza ni vema wakamwachia majukumu yote kocha wake mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems ili kumpa haki yake kama kocha ili timu iweze kufanya vizuri zaidi.

"Ni vizuri kama Simba wakamwachia kocha majukumu yote ya usajili ili kutoa uhuru wa kufanya kzi vizuri, nadhani itasaidia kuipa maendeleo Simba na kuifanua timu iwe imara" alisema.

Wakati Rage akitoa ushauri huo, kikosi cha Simba kinaondoka leo kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic