CECAFA imegwaya kuiadhibu Yanga na ikaishia kuitupia mpira TFF, huku
ikiwafungia Gormahia miaka miwili kushiriki mashindano ya Kagame baada
ya wachezaji wake kugomea medali za mshindi wa tatu juzi Ijumaa.
Wachezaji hao waligoma kama njia ya kushinikiza uongozi wao uwalipe
posho mshahara wa mwezi mmoja wanaodai. Habari zinasema kwamba wachezaji
hao walicheza mechi dhidi ya JKU na kushinda mabao 2-0 na waliamua
kutogomea mechi ili wapate mgawo wao wagawane.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema; “Kocha wa Gor Mahia
naye alikuwa akitoa maneno ya matusi kwa marefa hilo tumeliona kwenye
ripoti hivyo tunataka kuonesha kwamba tuna misimamo na kwa kila timu
itakayofanya makosa tutaiadhibu.”
“Kuna timu ambayo haikushiriki ikiwa na imani kwamba tutashindwa
kufanya vizuri hilo litakuwa chini ya TFF na kama tukiandaa mwakani
wakajitoa hatuna mashaka tutaendelea kufanya mashindano bila kuangalia
ukubwa wa timu,” alisema Musonye akionekana kuitupia madongo Yanga.
Habari zinasema kwamba Musonye na kamati yake wameigwaya Yanga
kwavile kuna uwezekano mkubwa mashindano yajayo yakarudi Dar es Salaam
kutokana na hali ya uchumi ya nchi washirika.
Azam juzi ilitwaa ubingwa wa Kagame baada ya kuifunga Simba kwenye
fainali. Ilijipatia Sh68milioni ambazo watakabidhiwa kesho Jumatatu huku
Simba ikiambulia Sh45milioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nifundisho kweli kocha wao Kerr alimtukana lefa kwenye gemu Kati ya gor mahia vs vaips
ReplyDeleteSuala la Kocha Kerr kumtukana Refa, anapaswa kuadhibiwa Kocha kwa kuangalia Kanunu zinasemaje, huwezi kuiadhibu Klabu nzima. Suala la wachezaji kugomea kuchukua medali zao kwangu mimi sio kubwa kivile, kwakuwa walicheza mchezo hawakugomea kucheza, hivyo adhabu ya utovu tu wa nidhamu wa kutopokea zawadi zao, hili unawaonya tuu. Unawafungia miaka 2?? Lipi kubwa aliyegomea mchezo au aliyegomea kuchukua zawadi unayompa?? Je zile dollar 10,000 nazo wamegomea?? Kama wamegomea vyote tatizo liko wapi? Kama wamechukua pesa, na bado mnataka kuwaadhibu basi mngewaambia usipochukua medali na fedha ziacheni. CECAFA liangalieni vizuri jambo hili. Kocha mwenye matusi huyo muadhibuni yeye mwenyewe sio Klabu yake.
ReplyDeleteKwani wasema klabu inaadhibiwa kwa kosa la kocha? kanuni za CECAFA kwa kitendo cha kugomea meadali zinasemaje?
DeleteTotally hawa jamaa wamefeli tena wanazidi kufeli na tatizo mojawapo la Cecafa ni Musonye imefika mahali hili Shirikisho limekua kama Kampuni yake na mkewe hawa viongozi wa mashiriko ya soka nchi mbalimbali ya wanakula viposho vinavyotokana na deal anazopiga huyu bwana basi kwake wamekua kama mlenda hii Cecafa kwa mwendo wake East Africa TUTAPATA TAABU SANA kusogea kwenda kokote kwa ngazi ya vilabu Wala Taifa ni upuuzi mtupu uliopo pale.
ReplyDelete