STRAIKA aliyeng’ara na Simba kwenye Kagame, Meddie Kagere amesema
kwamba endapo wachezaji walioko likizo wakirejea kwenye timu hiyo
akiwemo Emmanuel Okwi na John Bocco kikosi hicho kitatisha sana.
Kagere ametua Simba hivi karibuni akitokea Gor Mahia ya Kenya ambayo
mashabiki wao mpaka leo hawaamini kilichotokea mpaka akawakimbia.
Amefunga mabao manne kwenye Kagame.
Raia huyo wa Rwanda ambaye jana Jumamosi aliondoka kwenda kwao
kukamilisha mambo yake amesema; “Unajua asilimia kubwa ya wachezaji
wengi ambao tulikuwa tunacheza ndiyo mara yetu ya kwanza kuwa hapa sasa
imechangia kwa namna fulani hivi kushindwa kupata kile ambacho
tunakitaka kwenye Kagame.”
“Ninaamini kwamba wakija wachezaji wengine walio mapumziko (Okwi na
Bocco) na kupata muda mzuri wa kujiandaa basi nikwambie tu hakuna ambaye
atakuwa na uwezo wa kutuzuia sisi kwa msimu ujao, niwaambie tu
mashabiki wasubiri,” alisema Kagere ambaye amezaliwa Uganda.
Kocha wa Simba, Masoud Djuma aliwapa mapumziko wachezaji waliotumika
kwa asilimia kubwa kwenye ligi wakiwemo Okwi, Bocco, Aishi Manula,
Haruna Niyonzima, Jonas Mkude na wengineo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 COMMENTS:
Post a Comment