July 8, 2018


Na George Mganga

Bao pekee lililofungwa mnamo dakika ya 66 na Rashid Mohamed limeipa nafasi Simba ya kufuzu kutinga nusu fainali ya michuano ya KAGAME.

Katika mchezo iliocheza leo dhidi ya AS Ports kutoka Djibout, Simba wameweza kuibuka na ushindi huo wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa.

Licha ya kufunga bao hilo moja, Simba waliweza kulisakana lango la wapinzani wao lakini umakini katika safu ya ushambuliaji imekuwa tatizo jambo ambalo limepelekea ushindi huo hafifu.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuuunga na Gor Mahia FC ya Kenya ambayo ilikuwa ya kwanza kufika hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vipers SC ya Uganda.

Baada ya mechi za leo, kesho tena kutakuwa na michezo mingine miwili ambapo Azam FC itacheza na Rayon Sports huku Singida United ikikipiga na JKU.


3 COMMENTS:

 1. Hii timu ya Djibouti ilikuwa ya kupigwa hata 4. Simba kuna shida ya namba 8, beki ya kati, na namba 6, na mbili

  ReplyDelete
 2. Wana Simba tusidanganye kwa Kocha Masoud Djumaa kuwa ana uwezo wa kutufikisha mbali kwenye michuano ya klabu bingwa ya Africa.....namwona bado sanaaa...tusije tukaibikaa huko mbeleni.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wewe ni Mamluki! Nenda kapambane na hali yenu huko kwenye mafuriko.

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV