July 17, 2018


Imeelezwa kuwa uongozi wa Simba upo kwenye mazungumzo ya kimyakimya na beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani, kwa ajili ya kumsajili.

Tetesi za Yondani kuanza kuhitajika Simba zimeanza tangu msimu wa Ligi Kuu Bara 2017/18 umalizike lakini umekuwa ukikwama kutokana na Yanga kuendelea kumsisitiza aendelee kubaki,

Baada ya mkataba wa Yondani na Yanga kumalizika, uongozi wake umekuwa ukimtaka avute subira kwa ajili ya kusubiria mambo yakae vizuri ili baadaye aweze kuongeza mwingine.

Lakini inaonekana kama Yondani amechoka kuvumilia ambapo inaelezwa amekuwa miongoni mwa wachezaji waliogoma kwenda Kenya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika akidai kupewa mkataba mpya.

Taarifa sasa zinaelewa Mabosi wa Simba walio na jeuri ya fedha za tajiri kijana na Bilionea, Mohammed Dewji Mo, wanaweza wakamalizana na Yondani muda wowote kuanzia sasa ili kumrejesha Msimbazi kwa ajili ya uzoefu wake katika mashindano ya kimataifa.

12 COMMENTS:

  1. KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANTA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanasema Yanga inakaribia ina matawi zaidi ya 170 nchi nzima na kila tawi lina wanachama 100 ni wakati sasa wanachama ambao ni wamiliki wa club kuwajibika kwa kuichangia team yao sio wawe wapiga kura na kwenda mahakamani.Ata serikali wamewaambia wao wanahaki ya 51% ya hisa katika club. Waache blah blah sasa ndio wakati wa kuonyesha kwa vitendo kama kweli club ni Mali yao.

      Delete
    2. KUFANYA VURUGU YOYOTE ILE NI UPUUZI TUSIWE HIVYO. TUJENGE USTAARABU WA KUHESHIMU VIONGOZI WETU WA KLABU. MPIRA NI MCHEZO WA STAREHE KUFANYA FUJO NI KUVUNJA AMANI KWENYE KLABU JAMBO AMBALO HALITAVUMILIWA HIVYO SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE.

      Delete
  2. KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANTA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!

    ReplyDelete
  3. Yondani hana jipya mnapoteza pesa bure au mshazoea 20% .

    ReplyDelete
  4. Yondani hana jipya? Hivyo pale yanga kuna beki gani anaweza kuvaa viatu vya yondani? Yondani ana mapya mengi na kama simba watamsajili basi wameramba dume.

    ReplyDelete
  5. ha ha haaaa sasa usajili umefikia patamu

    ReplyDelete
    Replies
    1. UKISIKIA WATU KUANDAMANA , NDO TUTASHUHUDIA SAFARI HII

      Delete
  6. Hajasaini mkataba...hakuna haja ya kufanya Fuji au kuandamana

    ReplyDelete
  7. Siyo kumsajiri, Bali kumrudisha kundini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic