July 8, 2018


Mabao mawili aliyofunga mshambuliaji mpya wa Simba, Meddie Kagere kwenye michuano ya Kombe la Kagame yamemtisha straika wa timu hiyo, Adam Salamba ambaye lengo lake ni kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

Salamba aliyejiunga na Simba hivi karibuni kwa dau linalotajwa kuwa Sh mil 40, mpaka sasa amefunga mabao matatu na kuwa kinara ndani ya kikosi hicho katika michuano ya Kagame ambayo kesho Jumapili inachezwa robo fainali.

Kwa mujibu wa gazeti la championi, Salamba ambaye ana rasta za kiduku kichwani alisema, kasi ya Kagere katika kutupia inaweza kumzuia yeye kutimiza ndoto zake za kuwa mfungaji bora wa Kagame lakini atakaza kuhakikisha anapambana na kufunga mabao zaidi kwenye mechi zinazofuata.

“Kikubwa namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufunga mabao matatu na nimejiandaa vizuri ila cha msingi ni kupambana na kuweza kufunga mabao na kuibuka mfungaji bora.

“Kasi ya Kagere imenishtua lakini nimejipanga kupambana, unajua yule ni mchezaji mkubwa na ana uwezo mzuri, pia ni ‘profesheno’ kikubwa nitapambana,” alisema Salamba.

4 COMMENTS:

  1. Moyo kama huo ndio utaonyanyua kiwango cha mnyama na kuwezesha mngurumo wake wa wa utisha kusikizana sio nyumbani tu bali kote Africa

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Hamna editing bora liende utafikiri mwandishi wa blog anafukuzwa .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic