July 10, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha JKU kutoka Zanzibar kimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya KAGAME kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 yaliyopatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Hatua hiyo ilikuja mara baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu tasa ya 0-0 baina ya timu zote mbili.

Baada ya kutinga hatua hiyo, JKU sasa itaungana na Simba ambayo lifuzu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Ports ya Djibout kucheza mchezo wa nusu fainali.

Wakati JKU wakifuzu kufika hatua hiyo, uongozi wa Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema ulikuwa unaisubiria timu yoyote baina ya Singida na JKU huku wakiahidi yoyote atakayepita watapambana naye bila kudharau.

Ikumbukwe Simba ndiyo mabingwa wa kihistoria katika mashindano haya wakiwa wamefanikiwa kutwaa ubingwa mara 6 kuliko timu zote zingine ukanda wa Afrika Mashariki na Kati,

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV