July 10, 2018Na George Mganga

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbas Tarimba, ametangaza kuachana rasmi na wadhifa huo.


Kwa mujibu wa Radio Uhuru, Tarimba amefunguka na kueleza kuwa kumekuwa hakuna maelewano baina yake na Makamu Mwenyikiti wa Yanga, Clement Sanga, ambaye ameivunja kimyakimya kamati hiyo ambayo ilipitishwa katika mkutano mkuu.

Kufuatia tukio la kuvunjwa kwa kamati, Tarimba amesema hawezi akawa na muda wa kuonana na Sanga kwasababu ameivunja kamati, na hata kama asingefanya hivyo asingekuwa tayari kutekeleza majukumu ya kamati hiyo.

"Waachane na mimi , mimi sina muda wa kuonana na Sanga waachane na mimi, yeye kwanza kamati kaisha ivunja na hata kama wasinge vunja mimi nisingeweza kufanya kazi nao" alisema Tarimba.

Mbali na kauli hiyo, Tarimba amekanusha uwepo wa taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kuwa kamati yake imelipa madeni ya fedha zote zilizokuwa ni malimbikizo ya madeni kwa wachezaji.

Tarimba ameeleza kuwa hakuna ukweli kuhusiana na hilo akiwahusisha viongozi wa Yanga kuwa wamekuwa waongo hivyo na kuwaomba waache masuala ya usanii kwa kuwa klabu hiyo ni taasisi kubwa.

"Wanayanga mnadanganywa Yaani wanayanga mnadanganywa mchana kweupe, Yanga tuna tamaduni zetu sio hizi, viongozi ni waongo ,nawaomba watulize akili zao wasaidie timu ,wengine ni wakubwa wanaongoza mpaka bodi ya ligi ,sasa watumie ukubwa huo kuipeleka Yanga mbele waache uongo uongo" alisema.


6 COMMENTS:

 1. Tatizo la Yanga ni huyu Clement Sanga amewaletea majungu kamati ya akina Tarimba sasa wanataka kuachia ngazi. Bakora zinanukia Jangwani.....wanayanga okoeni timu.....Sanga na kamati yote ya utendaji ijiuzulu na uchaguzi ufanyike ama sivyo tunaenda kushuhudia anguko kubwa la Klabu. Figisu figisu za Sanga, Nyika Lingalangala, lukumayi, na wengine katika genge la umoja wa matawi ya Yanga limewazuia kamati ya akina Tarimba kufanya kazi yao!

  Huyo Manji mwenyewe sio wa kurudi sasa hivi wala kesho timu itakuwa hii...WANAYANGA MFUKUZENI SANGA NA VIONGOZI WOTE WALIOSABABISHA TARIMBA NA KAMATI ILIYOUNDWA NA BARAZA LA WADHAMINI NA KUTHIBITISHWA NA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA....KUNA WATU WANATAKA KUITUMIA YANGA KUJINUFAISHA....MSIDANGANYWE

  ReplyDelete
 2. Haya majungu wanayafanya kwa nia ya kutaka kutengeneza mazingira ya kuitafuna pesa ya CAF

  ReplyDelete
 3. MTANDAO NA KUNDI LOTE LA AKINA SANGA JIANDAENI KULINDA NYUMBA NA MAISHA YENU YASIDHURIWE NA KUNDI LA MASHABIKI NA WANACHAMA WENYE HASIRA NA GHADHABU AMBAO WANAJUA YOTE YANAYOENDELEA KUIDHOOFISHA TIMU YAO....HAKUTAKUWA NA AMANI.....WAMEKAA KIMYA USIFIKIRI WANAFURAHIA....MNAWAONGEZEA HASIRA....SASA MWISHO UMEKARIBIA MFUKO WA GHADHABU UPASUKE, YATAKAYOTOKEA NI MAAFA!!!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wote hatujui ukweli hapo!viongozi wa matawi ndo wanaojua ukweli,na Manji anataka kufanya kazi na Sanga,,,,tarimba hamtaki manji,,tarima,selemani majd,ma akili mali ndo kundi moja,nyika,sanga ndo kundi la manji

   Delete
 4. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 5. Yanga watapata tabu sana!hivi kumbe hata madeni hawajalipa.Sasa hao wanaowasajili watawalipa kivipi!

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV