July 10, 2018


Kiungo wa timu ya soka ya Brazil,  Paulinho, ameondoka katika klabu ya Barcelona ya Hispania na kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya  Guangzhou Evergrande, ya China.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atarejea huko kwa mkopo baada ya kucheza kwa msimu mmoja nchini Hispania ambapo ada ya uhamisho haikutajwa.

Paulinho amecheza michezo  34 na kufunga mabao tisa wakati Barcelona ilipokuwa bingwa wa La Liga msimu uliopita na amecheza michezo yote mitano wakati timu ya Brazil iliposhiriki Kombe la Dunia mwaka huu nchini Russia.

Alipokuwa  Guangzhou Evergrande tangu 2015 hadi 2017 ameichezea klabu hiyo michezo 63.

Barcelona imethibitisha jambo hilo na kusema timu hiyo ya China inaweza kumchukua mchezaji huyo moja kwa moja kama ikitaka.

Akiwa nchini Russia kwenye Kombe la Dunia, Paulinho alifunga bao moja dhidi ya Serbia na alicheza dhidi ya Ubelgiji iliyowatoa katika mashindano hayo kwa kuwafungamabao  2-1.

Paulinho alijiunga na Tottenham akitokea Corinthians mwaka  2013 kabla ya kwenda 2015.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV