July 18, 2018


Wakati msimu wa Ligi Kuu Bara 2018/19 ukisubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka hapa nchini, Mkurungenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema ratiba ya mechi zote inatoka leo.

Wambura amesema ratiba hiyo imezingatia kila kitu ikiwemo uwepo wa michuano ya CAF pamoja na mingine ambayo inakuwa inafanyika nchini ili kuondoa muingiliano wa ratiba.

Mkurugenzi huyo ameeleza awamu hii wamejitahidi kuiweka ratiba katika mpangilio mzuri tofauti na misimu ambayo imepita ili kuepuka uvunjaji na kupunguza malalamiko kwa baadhi ya klabu.

Kikao na Waandishi wa Habari kitafanyika leo kwa ajili ya kuiweka hadharani ratiba hiyo ili klabu zote ziweze kuiona tayari kujipanga kwa mechi za msimu mpya.

Ikumbukwe Ligi Kuu itaanza mwezi ujao wa Agosti ambapo jumla ya timu 20 zitakuwa zinawania kikombe cha ligi tofauti na 16 zilizokuwepo awali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic