KISA KOMBE LA DUNIA, KOCHA ARGENTINA AFUTWA KAZI
Shirikisho la Soka la Argentina (AFA), wamekubaliana na Kocha Jorge Sampaoli kufikia tamati ya mkataba wao.
Sampaoli anaondoka Argentina baada ya kikosi chake kuboronga katika michuano ya Kombe la Dunia.
Imeelezwa pande zote mbili zimeelewana. Pia Kocha wa viungo na Kocha wa mafunzo ya video nao wameachia ngazi.
Sampaoli alikiongoza kikosi cha Argentina katika michuano hiyo mpaka hatua ya 16 bora na kutolewa nje na Ufaransa kwa kipigo cha mabao 4-3.
0 COMMENTS:
Post a Comment