July 16, 2018


Wakati msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ukikaribia kunako mwezi Agosti 2018, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza rasmi mazoezi leo Jumatatu.

Taarifa kutoka Simba zimesema wachezaji wote waliokuwa likizo wataungana kambini chini ya Kocha wake Msaidizi, Masoud Djuma kwa ajili ya msimu wa 2018/19.

Ikumbukwe wachezaji wengi walio sehemu ya kikosi cha kwanza waliondolewa kwenye michuano ya KAGAME kwa ajili ya kuwapa mapumziko baada ya kucheza mechi nyingi za ligi.

Katika mazoezi yatakayoanza leo, wachezaji hao wataungana kwa pamoja na walioshiriki KAGAME tayari kwa matayarisho ya vipute vya Ligi Kuu.

Simba ilifanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2017/18 ikiwa na alama 69 juu ya Azam na Yanga.

3 COMMENTS:

  1. Machungu ya Kagame yanatakiwa kuondoka Masoud Djumaaa!!! Tuna imani nawe

    ReplyDelete
  2. ACHA USHABIKI WA KIFALA WW MWANDISHI KILAZA

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV