July 19, 2018


Kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara 2018/19 unaotarajia kuanza Agosti 22 uongozi wa Mtibwa Sugar umetangaza kumrejesha Mshambuliaji wake wa zamani, Juma Luizio.

Mtibwa wamefikia makubaliano na Luizio baada ya kuchwa na Simba kutokana na mkataba wake kumalizika huku akishindwa kupata nafasi ya kucheza akiwa na wekundu hao msimu uliopita.


Simba walishinda kumuongezea mkataba Luizio baada ya kutoridhishwa na kiwango chake na badala yake sasa ameamua kurejea nyumbani kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

Kurejea kwa Luizio Mtibwa kunampa nafasi ya kubwa ya kufanya vizuri ndani ya walima miwa hao kama ilivyokuwa mwanzo kabla hajaondoka kuelekea mahala pengine.

2 COMMENTS:

  1. Bado hajaweza kutambua wapi anakosea lakini ni mchezaji ana nafasi na bahati ya kuchezeshwa mechi nyingi tu naamini atakuja kuwa mchezaji muhimu bado ni kijana. tumtakie kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. Hicho kichwa habari ni ushuzi mtupu kwani nani kati ya Luzio na Simba aliemtosa mwenzie?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic