July 9, 2018Kiungo Fabrice Kakule kutoka nchini Rwanda ameanza mazoezi na Simba.

Kakule aliyewahi kutamba na Rayon Sports na Kiyovu zote za Rwanda tayari ameanza mazoezi na Simba leo jioni.

Kiungo huyo aliyekuwa nahodha wa Kiyovu ameanza mazoezi akionyesha uwezo kama vile aliwahi kuichezea Simba.

Kakule alionyesha uwezo na kushirikiana na wachezaji wa Simba kama alikuwa mwenyeji.

Simba inahitaji kumuona kiungo huyo kiraka kabla ya kuchukua uamuzi wa kumsajili.

3 COMMENTS:

 1. Huwezi kuja kushangaa Simba ikibeba tena ubingwa kabla ya ligi kumaliza. Wapo kama waendawazimu wakati huu wakihangaika kutafuta wachezaji na pengine wapo watu wanaobeza lakini ikumbukwe simba tayari wana timu imara kabisa kibindoni na wanachofanya sasa ni kuwa na timu ya pili yenye uzito sawa na ya akina okwi au kuliko. Azam anaweza kuja kuwa mpinzani waukweli wa msimu unaokuja kwa simba lakini wasipokuwa makini yatawakuta yalayowakuta Singida msimu huu. Sina uhakika lakini inawezekana kabisa Simba wanazielewa mbinu za Mholanzi wa Azam vizuri zaidi kuliko Mholanzi anavyojielewa kwa hivyo subiri tuone kama atakuja na mbinu mpya msimu huu.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Jamani chama langu la msimbazi vipi tena? Nasikia huyu mkongomani bado ana mkataba unaoisha mwakani mwezi wa 7. Timu yake anayoichezea sasa hivi Kiyovu Sports ya Rwanda inataka kuipeleka Simba Fifa kuilalamikia kufanya mazungumzo na kumfanyisha mazoezi mchezaji wao ambaye bado ana mkataba....Jamani ehe pamoja na kwamba tuna shida ya wachezaji wa kigeni lakini tufanyeni mambo kwa weledi kidogo tusije kuingia kwenye matatizo, na hizi pesa za mwekezaji zitumiwe vizuri sio kwa pupa. Haya mambo kama ni kweli basi Simba tutaumia kweli na mkono wa Fifa

   Delete
 2. Jamani chama langu la msimbazi vipi tena? Nasikia huyu mkongomani bado ana mkataba unaoisha mwakani mwezi wa 7. Timu yake anayoichezea sasa hivi Kiyovu Sports ya Rwanda inataka kuipeleka Simba Fifa kuilalamikia kufanya mazungumzo na kumfanyisha mazoezi mchezaji wao ambaye bado ana mkataba....Jamani ehe pamoja na kwamba tuna shida ya wachezaji wa kigeni lakini tufanyeni mambo kwa weledi kidogo tusije kuingia kwenye matatizo, na hizi pesa za mwekezaji zitumiwe vizuri sio kwa pupa. Haya mambo kama ni kweli basi Simba tutaumia kweli na mkono wa Fifa

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV