July 9, 2018




Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephan Kebwe amewazawadia viwanja vya kujenge nyumba wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar baada ya hivi karubuni kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la FA. 

Mtibwa Sugar ilitwaa ubingwa huo wa Kombe la FA hivi karibuni baada ya kuifunga Singida United katika mchezo wa fainali uliofanyika hivi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid huko jijini Arusha.

Akizungumza katika hafla ya  kuwapongeza wachezaji hao wa mtibwa Sugar iliyoanfaliwa na uongozi wa timu hiyo na kufanyika usikuu kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam, Kebwe amesema kuwa ameamua kutoa zawadi hiyo kwa wachezaji hao kutokana na kazi kubwa waliyoifanya ya uwanjani na kuweza kuutangaza vema mkoa wa Morogoro.

"Zawadi hiyo naomba iwe chachu ya mafanikio mengine msimu ujao lakini pia kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano ya kimtaifa ambayo tutashiri baadaye mwaka huu.

"Mimi pamoja na Wanamorogoro wote tutaendelea kuwaunga mkono na watakapo fanya vizuri na kuulete sifa mko wetu basi tutaendelea kuwapongeza kama ilivyofanyika leo," amesema Kebwe.

Katika hatu hatua nyingine baadhi ya wchezaji wa timu hiyo wamepewa tuzo na uongozi wao kutokana na kazi kubwa walioifanya msimu uliopita na kuiwezesha kutwaa ubingwa huo wa Kombe la FA.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic