July 9, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Azam FC kimeibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la KAGAME.

Katika mchezo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa, Azam imejipatia mabao yote manne kupitia kwa straika wake aliye kwenye fomu hivi sasa, Shaban Idd.

Rayon Sports wao wamejipatia mabao yao mawili kupitia kwa Rwatubyaye Abdul na Manishimwe Djabel.

Ushindi huo unaifanya Azam iweze kutinga hatua ya nusu fainali kwa kuungana na Simba pamoja na Gor Mahia FC ambazo tayari zimefuzu tangu jana.

Kuanzia saa moja usiku huu JKU na Singida United nao watakuwa kibaruani kwenye Uwanja wa Taifa kusaka mshindi mwingine atakayeungana na Azam pamoja na timu tajwa juu katika nusu fainali ya KAGAME.

1 COMMENTS:

  1. Huyu dogo ndiyo straika bora nchini anawazidi, boko, okwi, na chirwa sema watu tumekariri majina makubwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic