July 10, 2018


Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma, raia wa Burundi, ametaja sababu za beki Muavory Coast, Pascal Serge Wawa kutokuwa na kiwango bora kwamba ni kutokana na kutocheza muda mrefu.

Wawa ambaye ametua Simba hivi karibuni kwa kufanyiwa majaribio ya kusajiliwa kikosini hapo, ameonyesha kiwango cha chini katika michuano ya Kombe la Kagame.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Djuma amesema kuwa, beki huyo anashindwa kuonyesha kiwango chake kutokana na kutopata muda mwingi wa kucheza.

“Shida yake hakucheza kwa muda mrefu kutokana na kumaliza mkataba wake, ndiyo maana inaleta matatizo kwake ya kutocheza vizuri.

“Naamini muda ukiendelea kusonga mbele anaweza akawa vizuri baada ya kupata muda wa kucheza, tutaona huko mbele. Ni miongoni mwa wachezaji wazuri ambaye ana uelewa wa haraka unapomwambia kitu,” alisema Djuma.

4 COMMENTS:

  1. Duuuh! Haya bwana,usajili wa kukomoana ndo unavyokuwaga. Mnachukua magalasa badala ya wachezaji kisa alitakiwa na upande wa pili, haya sasa ooooh apewe muda....muda gani! Huo mkenge tayari.

    ReplyDelete
  2. Tulia wewe acha papala mpira sio mdako tuache na wawa wetu sisi nyie pambaneni na hali yenu. Nasema mtapata Tabu Sanaaa nyie gongo wazi 😁😁😁

    ReplyDelete
  3. Ni miongoni mwa wachezaji wazuri ambaye ana uelewa wa haraka unapomwambia kitu,”.........lakini kuna ukomo katika soka pale ambapo roho i radhi lakini mwili ni dhaifu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Drogba alicheza kiushindani mpaka miaka 34, tena akiwa striker. Miaka 32 sio kitu kwenye soccer. Mcheki CR7 na miaka yake 33

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic