LIVE KUTOKA AIRPORT DAR: RAIS MAGUFULI AKIPOKEA NDEGE MPYA BOEING 787-8
RAIS Dkt. John Magufuli leo Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania. Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana leo ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.
Waache watu waseme watakavyo kuhusu Magufuli kwakuwa sisi Watanzania unafiki tumeuweka mbele kuliko ibada, uzandiki ni vitu vya kawaida katika masiaha yetu ya kila siku, Njia za mkato za kiujanja ujanja na za kitapeli za kujitafutia riziki au maendeleo kwetu sisi Watanzania ni tamu kuliko sukari, Uongo,uoga,Uthubutu wa kutofanya vitu vikubwa vya maendeleo kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe binafsi na nchi yetu kwetu sisi Watanzania kama tumerogwa. Lakini wakati huohuo ni jambo la kushangaza sisi Watanzania ni majasiri tena wa ajabu wa kutengeneza na kufanya mambo ya hovyo. Hebu fikiria yule jamaa aliejiunganishia bomba la mafuta kwenye nyumba yake kutoka mkondo mkuu wa kupitishaia mafuta wa Taifa? tuachane na masuala ya ndege, ni hili suala la Reli ya kisasa. Uganda,Rwanda,Burundi congo DRC,Zambia hizi nchi zote hazina bahari na njia rahisi duniani ya kusafirisha mizigo mikubwa kwa masafa ya mbali hasa continent to continent ni njia ya bahari. Tanzania zamani sana ingeweza kuishi kwa kutegemea banadari zake tu kama kungekuwa na wathubutu wa fikra na matendo ya kijasiri kwa ajili ya maendeleo ya nchi na watu wake. Lakini la kushangaza tangu Magufuli alipoamua kuchukua hatua ya kujenga Reli kumekuwa na Genge la la watu hasa wanasiasa na wengine ndani ya chama chake wanaompiga vita na kumpinga na kusamabaza maneno ya hujuma juu ya mradi ule wa Reli ambao kwa hakika utakapokamilika ni ukombozi kwa mtanzania. Wakati mwengine mtu unakaa unajiuliza hivyo mpaka lini sisi watanzania tutakuwa watu wa kukaa na kulalamika? Ule mradi kama ungekuwa unajengwa nchi nyengine mfano China basi wananchi wake wangekwenda kujitolea kufanaya kazi bure ili ukamilike kwa haraka. Hakuna mtu mkamilifu hapa duniani kwakuwa hata baadhi ya mitume tena wakubwa kwa rank mbele ya Mungu kuna sehemu waliteleza katika matendo yao. Na Magufuli kama mwanaadamu wa kawaida bila shaka hatakosa mapungufu na ndio maana hata yeye mwenyewe husisitiza na kuwaomba watanzania wamuombee kwa Mungu kumuongoza katika kazi yake. Ila watanzania tumepata kiongozi wa maana ni Jembe hasa.Ni kiongozi jasiri wa kufanya mambo makubwa ambayo kwa watanzania wengi tuliozoea kuongozwa na viongozi waoga na wanafiki kwetu sisi huona ni kama ndoto kufanyika vitu anavyovifanya Maghufili. Hata mpira wetu kama TFF ingekuwa taasisi ya serikali basi hivi sasa tungekuwa tunazungumza vitu vyengine kabisa. Usuhuba wa Maghufuli na Nape tangu harakati za kampeni mpaka anakuwa raisi lakini alipoona anaelekea siko akampiga na chini bila kujali urafiki wao. Usuhuba wa Maghufuli na mwigulu mchemba tangu kampeni za uchaguzi mpaka wakati wa uraisi lakini Magufuli alipoona wizara anayoiongoza Mwigulu haipo sawa muheshimiwa raisi wala hakumumunya maneno alimpiga na chini Mwigulu kwa mslahi ya watanzania sasa watanzania tunataka kiongozi wa namna gani? Labda tunataka kiongozi wa kuja kututadanganya na kututoreshea rasilimali zetu?
ReplyDelete