BABA WA PATRICK ANENA MAZITO MSIBANI -VIDEO
MWILI wa MAREHEMU Mtoto Patrick Peter, jana umepumzishwa katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar baada ya kukamilishwa shughuli za kuuaga mwili huo katika Viwanja vya Leaders Club ambapo ambapo baba wa marehemu Patrick Peter Zacharia alinena mazito juu ya mtoto wake huyo.
Zacharia alipata nafasi ya kutoa neno ambapo alitaka Watanzania kutokuwa na mkanganyiko juu ya mtoto huyo kutokana na maneno ambayo yalizuka katika mitandao ya kijamii kuhusu baba mzazi wa Patrick.
“Patrick ni mtoto wangu kabisa na Rose ni mke wangu ambaye nilifunga nae ndoa na kukabidhiwa na wazazi wake kwahiyo hakuna mtu yeyote ambaye ataingia katikati na kusema lolote najua Patrick ametokea wapi mpaka kuingia kaburini,” alisema Zacharia.
Baba mzazi huyo alisema kuwa Patrick kama Mungu akimuwezesha kufungua macho alikuwa ni rafiki yake sana mpaka kufikia hatua ya kumuombea usiku pindi wanapopumzika.
Peter ambaye ni baba mzazi halisi wa Patrick ambaye alifunga ndoa na Rose Alphonce ‘Munalove’ wameungana jana kwa pamoja kuupumzisha mwili wa mtoto wao baada ya mkanganyiko wa baba mzazi wa mtoto huyo.
Awali kulikuwa na mtafaruku kati ya Muna na mumewe Zacharia kwa takriban siku tatu tangu Patrick afariki dunia nchini Kenya alipokuwa amekwenda kutibiwa hivi karibuni.
Hakuna mwanamke hapo ...
ReplyDeleteYaani wanajiita wasanii na maisha yao ni ya kisanii sanii tu.
DeleteMaisha ya kwenye mitandao na vyombo vya habari lakini ukijua uhalisia wa maisha yao ni aibu tupu.
Huna mke hapo
ReplyDelete