July 22, 2018



Kocha George Lwandamina amesema kama Simba wamefanikiwa kumnasa Cletus Chama, basi wamelamba dume.

Lwandamina raia wa Zambia aliyewahi kuinoa Yanga, ametoa sifa kwa kiungo huyo mpya wa Simba kwamba ni mchezaji hatari.

Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Lusaka, Zambia, Lwandamina amesema Chama ni mchezaji mwenye kasi na mzuri wa kuchezesha timu.

“Kabla sijaja Yanga alikuwa ni mchezaji wangu katika kikosi cha Zesco. Niliporejea Zambia nilimkuta amehamia Dinamo.

“Lakini Chama ni mchezaji mzuri sana, ana uwezo mkubwa wa kuichezesha timu na kutengeneza nafasi bora,” alisema.

Simba imemnasa kiungo huyo na jana alifuzu vipimo vya afya akiwa tayari kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara.

1 COMMENTS:

  1. Huyu jamaa anaonekana kuujua mpira. Acha tuone.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic