MADRID YAMTAKA RONALDO KUFANYA HILI KABLA YA KWENDA JUVENTUS: TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMAMOSI
Real Madrid inamtaka mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo kwamba hajalazimishwa kuondoka katika klabu hiyo iwapo mchezaji huyo wa Ureno ataelekea Juventus. (Mail)
Manchester United inataka kumsaini upya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 lakini wameambiwa kwamba kumekuwa na mazungumzo mazuri kuhusu uhamisho wake kuelekea Juve. (Independent)
Paris St-Germain iko tayari kulipa dau la £100m ili kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 27. (Goal)
West Ham iko tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ufaransa na Marseille Dimitri Payet kurudi mjini London iwapo atakubali kupunguza mshahara wake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliondoka katika klabu hiyo akiwa amekasirika yapata miezi 18 iliopita. (Mirror)
Jack Wilshere amefanya ukaguzi wa matibabu katika klabu ya West Ham huku klabu hiyo ikitaka kumsajili kiungo huyo aliye huru kwa kandarasi ya miaka mitatu na mapato ya £5m. (Times - subscription required)
Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha amekataa ombi la kumpatia mshahara wa £120,000 kwa wiki katika klabu hiyo.
Kutoka BBC
Tottenham, Everton na Borussia Dortmund wameripotiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Ivory Coast. (Sun)
Kombe la Dunia2018: Mambo muhimu unayofaa kujua robo fainali
Manchester United wamewaorodhesha mabeki wanane ambao inataka kuwanunua na watalazimika kulipa dau la kuvunja rekodi ili kuwa na fursa ya kuwasajili baadhi yao.. (Express)
Arsenal imeanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Sevilla na Ufaransa Steven N'Zonzi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 awali aliichezea Blackburn na Stoke. (Sky Sports)
Everton wameonyesha hamu yao katika kumsajili mshambulikaji wa Barcelona na Uhispania Paco Alcacer, 24. (Sport)
Kiungo wa kati wa Southampton na Uholanzi Jordy Clasie, 27, yuko tayari kurudi katika klabu yake ya zamani Feyenoord. (Sun)
Saint-Etienne wameimarisha ombi lao la mshambuliaji wa Sunderland na Tunisia Wahbi Khazri, 27, licha ya ushindani mkali kutoka kwa klabu ya Ligue 1 Rennes. (L'Equipe - in French)
Kiungo wa kati wa Sunderland Yann M'Vila, 28, huenda akarudi Uingereza.
0 COMMENTS:
Post a Comment