July 7, 2018



Na George Mganga

Ni rasmi sasa klabu ya Singida United imefanikiwa kunasa saini ya miaka mitatu na aliyekuwa kipa wa Njombe Mji FC, David Kisu.

Mbali na kuichezea Njombe Mji, Kisu aliwahi kuwatumikia mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 Simba SC ya jijini Dar es Salaam akiwa kama kipa wa akiba.

Kipa huyo alipaswa kutambulishwa mapema kabla ya michuano ya KAGAME lakini usajili wake ulichelewa kutokana na kukamilisha baadhi ya mambo kwenye mkataba wake ambayo tayari yameshafikiwa mwafaka.

Usajili wa Kisu kujiunga Singida unaifanya timu hiyo kuwa na walinda milango watatu hivi sasa ambapo wwaliopo ni Ally Mustapha na Manyika Peter Jr.

Singida wamezidi kuendelea na usajili kwa ajili ya kukisuka upya kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi (2017/18) utakaokuwa na idadi ya timu 20.

1 COMMENTS:

  1. Ni vema uliona na kulijua hilo Simba sc maana majuto ni mjukuu na kiukweli Wawa hawezi kukidhi kwa mechi hzi chache alizo perform ckulizika na kiwango chake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic