July 17, 2018


Wakati Yanga ikiwasili salama huko Nairobi jana, mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Ally Mayay amesema kikosi hicho kimeenda bila maandalizi ya kutosha.

Mayay ameeleza kuwa Yanga imefanya maandalizi ambayo hayaridhishi kwa ajili ya mchezo huo ambao ni wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Julai 18 2018 dhidi ya Gor Mahia FC.

Mayay ambaye ni Mchambuzi wa Masuala ya Soka hivi sasa, amesema Yanga imeenda Nairobi bila kuyapa uzito mashindano hayo kutokana na mechi za kirafiki ilizocheza kutoenda sawa na ukubwa wa mchezo huo dhidi ya Gor Mahia.

Mchezaji huyo wa zamani ndani ya Yanga, anaamini utakuwa ni mchezo mgumu kwakuwa timu haijakaa sawa na imeuchukulia mchezo huo kama wa kawaida akisema kwa namna moja ama nyingine itawapa Yanga changamoto kubwa.

Katika michuano ya KAGAME iliyomalizika wiki jana jijini Dar es Salaam, Mayay amewaelezea Gor Mahia kuwa wameimarika zaidi akisema watakuwa na moto walioondoka nao kwenye mashindano hayo tofauti na Yanga waliocheza michezo ya kirafiki ya kawaida.

"Yanga imeend bila maandalizi ya kutosha, ukiangalia mechi za kirafiki walizocheza haziendani na uzito wa mechi hiyo. Gor Mahia wameondoka kushiriki KAGAME hivyo wataingia kucheza wakiwa wako vizuri zaidi ya Yanga ambao itakuwa changamoto kwao" alisema.


7 COMMENTS:

  1. HIVI YANGA MBONA MNATUAIBISHA HIVI.....MIMI NITAANDIKA BARUA TFF ILI ITOE ONYO AMA KUWAADHIBISHA VIONGOZI WA TIMU ZOTE ZINAZOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA, KAMA HAKUNA MAANDALIZI YA KUTOSHA , NA KUWA KAMA WACHEZAJI HAWAPEWI MAANDALIZI MAZURI, MAZOEZINI, MALIPO NA MOTISHA NZURI, SAFARINI KUKOSA WACHEZAJI MUHIMU, MWISHONI KATIKA MECHI AMBAPO WANAWAKILISHA NCHI NA KUBEBA BENDERA YA NCHI.....MWISHONI KUISHIA KUFUNGWA AIBU SIO KWA YANGA TU BALI TAIFA ZIMA...RAISI MAGUFULI NAKUMBUKA ALISEMA IFIKE MWISHO TIMU ZETU ZISIWE ZINAISHIA KUFUNGWA FUNGWA TU, NI AIBU SANA...IFIKE MWISHO SASA. YANGA HAWAKUSHIRIKI CECAFA WAKISEMA WACHEZAJI WAO HAWANA MIKATABA, NA WAMEPEWA RUHUSA YA KUPUMZIKA, SASA CAF IMEFIKA NAPO BADO KUMBE HATA MIKATABA HAWAJAPEWA NA WENGINE WANAGOMA, MAJINA YA WACHEZAJI WATATU YAMECHELEWA CAF, HAYA BADO USAJILI UNASUASUA HUU NI UPUUZI MKUBWA....HAIVUMILIKI LAZIMA VIONGOZI WOTE WAJIUZULU.....TUNAKWENDA KUIAIBISHA NCHI...KUNA HAJA GANI YA YANGA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYA IKIWA KWAMBA WANAENDA KUPELEKA KIKOSI KISICHO IMARA...WATANZANIA IMEFIKA WAKATI TUSIWE TUNATEGEMEA MIUJIZA, AU BAHATI...MPIRA NI SAYANSI NA MAANDALIZI, NA MOTISHA KWA WACHEZAJI NA BENCHI LA UFUNDI.....USANII NA USWAHILI SWAHILI UFIKE MWISHO....WAPENZI WA SOKA TANZANIA TUMECHOKA KUWA WASINDIKIZAJI NA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU JAMANI......

    ReplyDelete
    Replies
    1. JUMATANO KESHO TIMU INACHEZA KULE KENYA ACHENI KULETA MANENO YA KUWAKATISHA TAMAA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA TIMU YETU WOTE INAYOWAKILISHA NCHI MUHIMU KUWATIA MYO NA KUWAOMBEA WAFANYE VIZURI

      Delete
    2. This comment has been removed by the author.

      Delete
    3. Hao TFF wanazisaidia kitu gani hizo timu

      Delete
  2. Nawatakia Yanga kila la kheri - KIMSINGI GOR MAHIA WAMECHOKA SANA WAMECHEZA MECHI NYINGI SANA MFULULULIZO KWAHIYO YANGA WANAWEZA CHUKUA HIYO ADVANTAGE

    ReplyDelete
  3. Yanga ingelishiriki mechi za kagame wangepata fursa kubwa ya kujipima, lakini walipatwa na woga walipogunduwa wapo katika kundi la Simba timu ambayo imechezesha zaidi wachezaji wa kikosi cha pili na wakaogopa kipigo hivo kuamuwa kujitoa kabisa na huku ikijinadi kusajili bora kuliko wale wa Simba na sasa wapo Kenya bila ya matayarisho huku wakizidi kujivuruga

    ReplyDelete
  4. Yanga mwaka huu acha tumrudishe Yondani Nyumbani tu njaa hajazoea nyumbani kwao Simba hakuua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic