July 17, 2018


Na George Mganga

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga na sasa Mkufunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Jonas Tiboroha, amepingana na uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha ongezeko la wachezaji wa kigeni.

Siku kadhaa zilopita TFF kupitia Rais wake, ilitangaza kuongeza wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu Bara kutoka 7 mpaka 10.

Uamuzi huo wa TFF umemfanya Tiboroha aibuke na kupinga suala hilo akiamini kuwa itakuwa changamoto kubwa kulinda vipaji vya wazawa kwa faida ya timu ya taifa.

Kwa mujibu wa Radio One kupitia Spoti Leo, Tiboroha ambaye aliwahi kuwa na wadhifa wa Ukatibu ndani ya Yanga wakati Yusuph Manji akiwa Mwenyekiti wa klabu, amesema si sahihi kwa TFF kufanya vile akieleza si wakati mwafaka kwa sasa.

Mkufunzi huyo wa UDSM ameshindwa kuelewa kwanini TFF imefikia huko wakati soka la Tanzania bado ni changa kiasi cha kwamba itawapa ugumu zaidi wachezaji wa hapa nyumbani kutoka kimpira.

Tiboroha amefunguka mengi huku akisema vipaji vya vijana havitoweza kuonekana baada ya ongezeko hilo kupitishwa na TFF huku akieleza haikuwa wakati sahihi kwa sasa.

"Sijui soka letu linaelekea wapi, hii itakuwa changamoto kubwa kwa wazawa maana vipnaji vyao havitaweza kuonekana. Haukuwa wakati mwafaka kufanya maamuzi hayo" alisema.

5 COMMENTS:

  1. Hoja isio na mshiko hata kidogo sitaki kusema ya hovyo nikaja nikaonekana mkosefu wa maadili. Unaposema kulinda vipaji unamaanisha nini? Kukilinda kitu bila ya kuwa na mikakati ya aina yoyote ile ya kukiongezea thamani kuna faida gani? Anasena soka la Tanzania bado changa? Na Kylan Mbape nae ni mchanga sana hakupaswa kujumuishwa kuchezea kombe la Dunia? Na hii kasumba watanzania ya kusingizia umri kwa kila kunapo changamoto tumeipata wapi? Wale Wasudani Kusini ni taifa jipya lakini kunako uhai kama tupo basi watashiriki kombe la Dunia na sisi bado tunasubiri kulinda vipaji vyetu. Ikiwa tuna maprofesa waoga basi si shangai kuona tuna jamii yenye vijana wenye kukosa uthubutu na ujasiri wa kujitafutia maendeleo. Mimi nnaimani vijana wetu umefika wakati wa kuwatafutia changamoto kwa faiada ya maendeleo yao wenyewe binafsi kazi ni kwa makocha hasa wazawa kuwafunda vijana wetu jinsi ya kupambana kuhakisha hawawi wasindikizaji kwani hata wazo la kuanzisha vyama vingi Tanzania halikuwa suala rahisi lakini Baba wa taifa mwalimu Nyerere miongoni mwa wanaume wa kweli wa kitanzania hakuwa na hofu za kipuuzi ulipofika wakati wa kuchukua maamuzi magumu alisisitiza wakati umefika. Na licha yakuwa na matukio ya hapa na pale kuhusiana na vyama vingi lakini Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Africa nufaika wa mfumo wa vyama vingi. Pengine bila ya vyama vingi hata Magufuli asingethubutu kuwa Raisi. Pressure na ushindani wa kisiasa kutoka vyama vya upinzani imeiyamsha CCM na kutafuna viongozi walio sahihi kwa manufaa ya nchi na wananchi wake na sio chama na viongozi wake na familia zao peke yake. Siku zote...You can't be a brave if you have only had a wonderful things happen to you in your life. Watanzania tuache kulalamika badala yake tuna takiwa kubadilika na kuwa watu wa kutoa mawazo ya kimkakati ya kutafuta ufumbuzi wa vitu vinavyotukwamisha kupiga hatua.

    ReplyDelete
  2. Wazee wa kupinga, bado akilimali ����

    ReplyDelete
  3. Napata shida sana na pengine nitaendelea kupata taabu sanaa kuelewa kwa namna gani vipaji vya wachezaji wazawa vitapotea na timu ya taifa itaadhirika simply kwa kuongenza wachezaji wa kigeni kwenye ligi?...Professor na elimu yako unashindwa kutupa hoja or technically kwa nini wazawa vipaji vitapotea?..VPL imeongenzeka timu 20...Na ktk timu hizi ni timu 2 hadi 4 ndio zitakozoweza kusajili wachezaji zaidi ya 7.Team 16 zilizobaki sidhani zinaweza kusajili wachezaji wa kigeni zaidi ya 3.kwa mantiki hii ukichukulia Mtibwa ambayo falasafa yao ni wachezaji wazawa watupu ndio itakayowapa changamoto timu yenye wachezaji wengi wazawa na kwa maana hiyo watajituma kuwaonyesha mashabiki kuwa wana vipaji na wanaweza.Ndio tutakapopata vijana hodari wa kuchezea timu ya Taifa...sasa hapa vipaji vya wazawa vinapoteaje?Inabidi vijana waongozwe kuwa pesa si kila kitu Bali malengo yako nini kabla hujafikisha umri wa miaka 24?
    Tatizo la wachezaji wazawa hawajitumi kikamilifu....malengo yao tunayosikia kila siku ni kuwa kwenda kucheza soka nje lkn ni wangapi wameenda huko na kushindwa majaribio?...sababu ligi yetu ina wachezaji wengi wa kigeni?
    Tunapaswa kuwaambia ukweli wachezaji wetu wazawa wapambane na ieleweke klabu zinahitaji wachezaji wapambanaji ili kuitanganza nembo yake kwa ajili ya biashara na mpira siku hizi ni pesa.Kama unajaza wachezaji wanaocheza na jukwaa na hawaleti matokeo basi kwa nini usitafute nje ili timu ipate matokeo isiwaangushe wadhamini,wawekazaji na wana hisa ndani ya klabu?
    Profesa bado napata taabu sana kukuelewa na hoja yako ambayo naiona ni dhaifu.

    ReplyDelete
  4. mtibwa siku zote inafanya vizuri kwa kutumia wachezaji wazawa na kila ligi ikiisha timu kubwa zinaenda kusajili Mtibwa wachezaji wazawa watapata changamoto maana si timu zote zina uwezo kusajili wachezaji wazawa hawa ndio wasomi mnaosema ndio wanastahili kuongoza mpira kisa wamefika la saba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic