July 10, 2018


Wakati michuano ya Kagame ikifika hatua ya nusu fainali hivi sasa katika jiji la Dar es Salaam, mchezaji wa zamani wa Yanga, Yusuph Macho, amefunguka na kuzungumzia machache kulingana na vipaji vya wazawa.

Kwa mujibu wa E Sports kutoka EFM, Macho ambaye aliwahi kung'ara na klabu ya Yanga, Mtibwa pamoja na Simba, amesema kuwa kwa mwenendo namna unavyoenda hivi sasa wachezaji wazawa wamejitahidi kuonesha uwezo wao vizuri.



Straika huyo wa zamani amewaelezea Adam Salamba, Mohamed Rashid na Marcel Kaheza kuwa ni wachezaji ambao walimkosha kwa kuonesha kiwango kizuri katika mechi ya Simba dhidi ya AS Ports ya Djibout.

Mkongwe huyo anaamini kuwepo kwa wachezaji wa kigeni inawasaidia zaidi wazawa kujituma Uwanjani kutokana na changamoto ambazo wanazipata ndani ya Uwanja na kuwafanya wapambane.

Macho amesema wachezaji hao walicheza wakiwa na mawasiliano mazuri kiasi cha kwamba taswira tofauti inaanza kuonekana kwa wazawa wa hapa Tanzania tofauti na ilivyozoeleka kuwa lazima wageni wafanye vema.

4 COMMENTS:

  1. Mbona hiyo picha ni ya MTU mwingine ambaye hausiani na habari husika? Umeshaanza kuleta siasa za CUF hapa!!

    ReplyDelete
  2. Salamba ni Adam, sio Mohamed. Mnakosea majina ya watu kama polisi!

    ReplyDelete
  3. Hiyo picture co ya yusuph macho musso rwenda

    ReplyDelete
  4. picha ya Mtatiro wa 'CUF', mnaweza kuweka ya macho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic