July 10, 2018


Uongozi wa Stand United kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Mbasha Matutu, amesema kuwa mchezaji, beki Ally Ally aliyesajiliwa na KMC FC kwa kusaini mwaka mmoja bado ni mchezaji wao.

Matutu ameeleza Ally ameondoka Stand akiwa amebakiza miaka miwili ambapo mkataba wake ulikuwa ni wa miaka mitatu hivyo ni mmoja pekee ambao ametumikia.

MWenyekit huyo amefunguka na kusema amesikitishwa na mchezaji huyo kuondoka Shinyanga na kutimkia Dar es Salaam kisha kumalizana na KMC ambayo imepanda daraja kushiriki Ligi Kuu Bara.

Mbali na hilo, Matutu ameelezea pia suala la Ally ambaye alilalamika kuwa hajalipwa mshahara wa miezi mitatu na Stand, akisema kuwa halina ukweli kuwa kila mchezaji amekuwa akilipwa kwa wakati.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa Ally alikuwa alikuwa akipata mshahara wake kama kawaida na hakuna deni lolote ambalo alikuwa anaidai klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic