July 17, 2018


Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kushuka dimbani kesho kukipiga dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, amesema watahakikisha wanaimaliza timu hiyo.

Zahera ambaye amechukua mikoba ya Mzambia George Lwandamina, amesema watatumia udhaifu wa Gor Mahia waliouonesha katika mashindano ya KAGAME yaliyomalizika wiki jana jijini Dar es Salaam.

Kocha huyo ameeleza kuwa Gor Mahia wana timu ambayo imekaa muda mrefu lakini mapungufu yao yapo katika safu ya ulinzi, hivyo watatumia mwanya huo kupata matokeo.

Zahera amesema wapinzani wao wapo vizuri ila kupitia nafasi ya ulinzi bado ina shida kidogo kwao na amaanini wanaweza kuitumia ili kupata matokeo chanya

Ikumbukwe Yanga haijapata ushindi wowote tangu kuangukia mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa Ligi ya Mabingwa Afrika na kesho watajituma kuhakikisha wanapata matokeo.

Yanga imeenda suluhu pekee ya 0-0 dhidi ya rayon Sports ya Rwanda huku ikipoteza mchezo mmoja dhidi ya MC Algeria ya Algeria kwa kufungwa mabao 4-0 ugenini.

4 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANYA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!

    ReplyDelete
  4. Yanga Nguvu moja. Yanga hawapo vibaya wa hivyo kitimu ila upande wa mgogoro. Hata binaadamu wa kawaida anapofilisika kitu cha kwanza kitakacho pata mtikisiko ni Ndoa. Na ndio pale wazee wa kifamilia hupendelea mwanafamilia wao kufunga ndoa na mtu sahii mwenye mapenzi na ubinaadamu sio kitu. Mvumilivu wa majaribio katika maisha nakadhalika nakadhalika. Kwa hiyo Yanga itaendelea kuteseka kwa sasa lakini sio jambo zuri hata kidogo kwani wachezaji wanaokosa uzalendo kuipigania yanga ni wachezaji hao hao watakaosa uzalendo kuipigania Taifa Stars. Kwa hivyo elimu ya uraia kwa wachezeji wazawa ndani ya Yanga ilihitajika badala ya kuliachia jahazi kuzama.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic