July 18, 2018


Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, leo atakosekana katika benchi la ufundi la timu yake kutokana na kukosa vibali vya kufanyia kazi.

Zahera amekuwa akiinoa Yanga tangu achukue mikoba ya Mzambia, George Lwandamina, lakini mpaka sasa hajapatiwa vibali kitu ambacho kinamfanya aendelee kukosekana kwenye benchi la ufundi.

Taarifa kutoka kwa viongozi wa Yanga zinasema uongozi mpaka sasa unapambana kuhakikisha unapata vibali kwa ajili ya Zahera ili kuweza kutimiza majukumu yake kama Kocha kwa asilimia 100.

Yanga itakuwa inashuka dimbani leo kucheza mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Gor Mahia FC wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Zahera atakuwa jukwaani.

Kuelekea mechi hiyo tayari Zahera ameshakiandaa kikosi hicho ambacho kitaongozwa na Noel Mwandila kusukuma gozi dhidi ya wapinzani wao ambao mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini Kenya

5 COMMENTS:

  1. KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANYA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!

    ReplyDelete
  2. YANGA jamani vipi nyinyi viongozi? Mnakosaje kibali cha Kocha wiki zote hizi toka amekuja?

    ReplyDelete
  3. Yanga kuna uzembe unaendelea pale kwa upande wa viongozi si bure kha?

    ReplyDelete
  4. Hivi Zahera tangu ameanza kuifundisha Yanga bado anaendelea kaa jukwaani?Alifika kama mwezi tangu Lwandamini aondoke?

    ReplyDelete
  5. Shida ni uongozi,yimu yote ya uonhozi ndiyo shida.hivi wao hawajui hadi Leo kuwa mpira ni biashara? Kwa mini wanavunda sokoni hadi Leo,?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic