MWANDISHI AACHA KAZI SABABU YA MESSI
Wakati mashabiki wa soka duniani wakiendelea kufuatilia yanayojiri Kombe la Dunia Urusi, kwa mwandishi mmoja Rwanda, ni wakati wa kulipia gharama kutokana na ahadi aliyoitoa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka BBC, Rutamu Elie Joe alikuwa amewaahidi wasikilizaji akiwa hewani kwamba angeacha kazi iwapo Argentina wangekosa kushinda Kombe la Dunia mwaka huu.
Ndoto yao ilizimwa Jumamosi walipolazwa 4-3 na Ufaransa.
Mwandishi huyo anasema alitoa ahadi siku ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia na kusema ''Mwaka huu ndio Lionel Messi atachukua Kombe la Dunia.''
''Messi asipochukua Kombe la Dunia basi mimi naachana na hii kazi yangu ya utangazaji wa mpira pamoja na kufanya kazi katika kituo hiki cha redio."
Anasema kwake alikuwa analichukulia kama jambo la kawaida, kutoa ahadi tu lakini baadaye amekuja kuwajibishwa.
''Mimi nilikuwa nafikiria ni kawaida tu kama kipindi cha kawaida tu ambacho kimepita kumbe watu wamekirekodi na wakasalia kimya''.
0 COMMENTS:
Post a Comment