July 8, 2018


Wakati ikielezwa kuwa klabu ya Simba ipo kwenye mchakato wa kusaka beki mwingine ambaye ni mbadala wa Sergi Wawa, uongozi umeibuka na kukanusha taarifa hizo.

kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameibuka na kukanusha uwepo wa taarifa zilizoeleza kuwa klabu hiyo ina mpango wa kuachana na beki huyo kutoka Ivory Coast.

Manara amesema taarifa hizo zinapaswa kupuuzwa akieleza hazina ukweli wowote huku akimkingia kifua Wawa kwa kusema ni mapema sana kumhukumu kwasababu hajacheza kwa muda mrefu.

Mbali na suala la kutocheza kwa muda mrefu, Manara amefunguka na kusema kuwa klabu ya Simba ina imani naye hivyo haitowezekana ikaamua kuachana naye kwa mechi tatu pekee ambazo ameshacheza.

Wawa ambaye alitambulishwa hivi karibuni na uongozi huo katika makao makuu ya Simba yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam, ameanza kuhusishwa kuachwa ikiwa ni takribani wiki mbili tangu ajiunge na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18.

5 COMMENTS:

  1. Hii kisheria inaitwa MKANO WA MKANWA

    ReplyDelete
  2. Manara is most instant to speak for his team compared to all others to their teams, the abliest among teams' commentators. Those who used to ridicule him, are no longer heard

    ReplyDelete
  3. Kazi ya Msemaji wa Klabu ndio hii, kusemea klabu wakati muafaka sio kuacha watu kueneza uvumi halafu timu inaharibika. Wawa amesemwa kwa kushindwa kukaba ipasavyo kwenye mechi za Kagame. Moja ya mechi hizo ni goli la kusawazisha la Singida.Nimeangalia mara 4 video ya goli lile . Mchezaji aliyecheza ovyo na kusababisha goli lile alikuwa Muzamir. Badala ya kufanya clearance mpira wende mbali yeye akampasia adui na ilikuwa ndani ya robo uwanja wa golini mwa Simba. Hapo ndipo kosa kubwa lilipotokea. Wawa bado anajijenga kimwili. Ni beki mzuri ila tu kuna marekebisho kocha atamsaidia

    ReplyDelete
  4. Ni wapuuzi na wanafiki tu ndio wanataka kuwatoa Simba kwenye reli.Wawa ni defender anayetumia akili na nguvu kama enzi zile za Victor Costa.Si defender wa kubutua na mpira kwenda kuangukia Tandika sokoni

    ReplyDelete
  5. Wawa umri umemtupa tz ligi ngumu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic