July 21, 2018


Mabingwa wa Ligi Kuu Bara nchini, Simba SC, wameshusha kiungo mshambuliaji mpya kutoka Dyanamos FC ya Zambia, Chama Clatous na taarifa zinaeleza tayari ameshamalizana na mabosi wa klabu hiyo.

Ujio wa Clatous Simba umetokana na pendekezo la Kocha Msaidizi, Masoud Djuma ambaye aliomba asajiliwa kiungo mwingine ili kuja kukupa nguvu kikosi cha Simba kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema tayari Clatous ameshamwaga winno na atakuwa sehemu ya wachezaji wataokwea pipa kesho kuelekea Uturuki kuweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Simba imekuwa ikitumia jeuri ya fedha za tajiri Mohammed Dewji ambaye ndiye mwekezaji mkuu wa klabu hiyo sasa kusajili wachezaji ambapo imeamua kukipa upana mkubwa kwa ajili ya ligi na mashindano ya kimataifa.

Ujio wa Mzambia huyo unazidi kuongeza idadi ya viungo Simba ambapo baadhi wanaocheza katika nafasi hiyo ni pamoja na Shiza Kichuya, Jonas Mkude, James Kotei na  Mzamiru Yassin



7 COMMENTS:

  1. Simba wamedhamiria kufanya kweli. Ni kweli kabisa kuwa huyu kijan ni mchezaji wa kipolopolo. Wikipedia inaonesha yakuwa ni mchezaji wa Itihadi ya Misri ila hakuonekana kuwahi kuichezea hata mechi moja. Ni mchezaji mzowefu mtu wa kazi kweli.

    ReplyDelete
  2. Karibu simba clatous lakini usije ukawa kama mavugo sisi simba kauli mbiu yetu ni kazi tu

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...Hongereni Simba Nmepata Bonge La Mchezaji.
    Nakumbuka Kuwahi Kumshuhudia Akichezea Zesco Chini ya Lwandamina Wakiifunga Al Ahly ya Misri 4-3 Huku Yeye Akiwa Mchezaji Bora wa Mechi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hiyo mechi aliwapoteza sana waarabu ndio apooneka misri na Lwandamina alimpendekeza Yanga lakini waarabu walimuwai. Nafikiri Simba Kwa mara ya kwanza kusajili mchezaji mzuri baada ya Okwi

      Delete
  4. Kwa uelewa wangu Kauli mbiu ya simba "Simba yasonga mbele" . Hiyo ya hapa kazi tu ni ya kwenu hukohuko

    ReplyDelete
  5. Clatous Chota Chama a.k.a Triple C karibu Simba

    ReplyDelete
  6. Simba kama Pascal wawa atatengemaa na kuwa fiti kama wawa tunae mfahamu basi vilabu kama kina Almasry wasiombee kuja kukutana tena na Simba kwani watakuja kupata taabu sana. Simba walichofanya ni kukijaza nyama kikosi kilichofika kikomo katika mechi ya Almasry kwa upande wa mashindano ya Africa lakini kwa upande wa ligi kuu wamebeba kirahisi kabisa. Hapao utauona utofauti wa viwango kati ya ligi yetu na mashindano ya Africa. Simba haikuhitaji kusajili kama ingelikuwa kwa ajili ya ligi ya ndani tu kwani wachezaji waliokuwepo wangetosha. Lakini baada ya muda mrefu Simba kukosekana Africa imerudi, tena kwa malengo na mikakati mipya kabisa itakayotuma salamu tosha kwa vilabu vigogo wa soka barani Africa mwakani. Kuanzia midfield mpaka mbele hawa vijana kama watakuwa wazima wa afya na kucheza kwa maelewano simba itakuwa sio clabu ya kubeza hata kidogo. Kama Nicholasi Gayani ataendelea kuaminiwa namba mbili na kuimudu vizuri basi kapombe na Mzambia watasimama katikati. Kichuya,Kagere, okwi,Boko wakisimama kule mbele shughuli sio ndogo au itategemea ingizo jipya la akina kaheza,Salamba, Mohamedi Rashid watakavyoweza kula sahani moja na akina Boko nnaimani wanaweza wakijitambua ni vijana wadogo wana kasi na nguvu wana uwezo wa kufanya mazoezi maradufu zaidi ya wale waliowazidi umri na kuifanya simba kuwa na safu ya ushambuliaji ya maangamizi kuwahi kutokea . Muzamiru,said Ndemla, Mohamedi Ibrahim hawa vijana wanavipaji na uwezo mkubwa na hawana haja ya kusubiri ila ni kuanza mapambano sasa kuhakikisha wanakuwa bora na kuwa miongoni mwa wasiopishana viwango au kuwazidi wale wachezaji wanaohisi wana namba zao tayari. Wasiwasi wangu kwa Simba bado upo kwenye beki line hasa beki ya kati kwani kwasi yupo vizuri pembeni au wamrejeshe kwasi kati kama alivyokuwa akipiga mbao. Mlipili ni kijana mzuri ila anakosa nguvu ni tatizo la vijana wetu wa kitanzania kutohangaika kuijenga miili yao ikashiba kikazi. Beki wa kati kote Duniani anatakiwa kuwa mwamba yaani kuwa na mwili wa kibabe.Angepatikana beki mmoja wa kazi kweli kweli kuja kuongeza nguvu awe beki wa ndani au wa nje basi sio mbaya na akipatikana basi kwa namana ya usajili wa simba ulivyopangika vizuri ni kuja kuifurahisha Dream liner yetu kubeba timu ya ushindi barani Africa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic