MWENYEKITI WA MATAWI YANGA AMJIBU TARIMBA, ASEMA AMEPOTOSHA UMMA, MENGI AFUNGUKA
Na George Mganga
Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi ya klabu ya Yanga nchini, Bakili Makele, amefunguka na kupinga kile alichokieleza aliyekuwa Mwenyekiti wa kuivusha Yanga katika kipindi cha mpito, Abbas Tarimba, akisema ni amepotosha umma.
Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari, Makele ameeleza kuwa Tarimba ameudanganya na kuupotosha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga ameivunja kamati hiyo.
Makele amesema kuwa Sanga hakuvunja kamati hiyo bali ni uongo aliotamka Tarimba huku akimsema kuwa alikuwa anatafuta njia ya kutokea 'Kiki' badala ya kusema ukweli kuhusiana na kamati.
Aidha, Makele ameeeleza Yanga inahitaji watu ambao wanafanya vitendo na si maneno, kitu ambacho kinasababisha mambo kutoenda sawa, akieleza yawezekana Tarimba alishindwa kutimiza majukumu yake na kuamua kujitoa.
"Iweje huyu mtu ajitoe peke yake wakati wengine bado wapo? Kwanza amepotosha umma, Sanga hajaivunja Kamati kama alivyosema, klabu inahitaji watu wasio na maneno bali vitendo" alisema.
Mwenyekiti huyo ameshangazwa na kitendo cha Tarimba kuamua kujiondoa Yanga ilihali wengine wakiendelea kusalia kwenye kamati, kitu ambacho kwake kama Mwenyekiti wa Matawi kimemshangaza.
Ikumbukwe Tarimba aliteuliwa kukaa kwenye nafasi hiyo kufuatia Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika Juni 10 katika Bwalo la Polisi Oysterbay Dar es Salaam.
Mwache Tarimba aondoke Yanga itaendelea tuu bila yeye kwani wapo wenye uchungu na timu
ReplyDelete