July 11, 2018


Wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum kuivusha Yanga wakati wa mpito, Abbas Tarimba, akijiondoa kwenye nafasi hiyo, Mwenyekiti wa Matawi Yanga, Bakili Makele, amewasilisha kile alichokisema Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo kabla ya Tarimba kujivua wadhifa huo.

Makele amesema sababu zilizopoelekea Tarimba kujiondoa Yanga ni kutokana na Sanga kueleza kuwa Tarimba haitendei haki nafasi yake kama ambavyo kwa kushindwa kufanya lolote tangu akabidhiwe nafasi hiyo.

Mbali na kutimiza majukumu ya Kamati, Makele amefunguka kuwa Sanga alieleza Tarimba amedanganya kuhusiana na suala la kusema kuwa Kamati ya Usajili ameivunja akisema jambo hilo halina ukweli wowote.

Aidha Makele ameeleza pia Makamu Mwenyekiti wake Sanga amesema Tarimba hakuwa anatimiza wajibu wake katika kuisaidia Yanga kwani alikuwa akijinasibu kuhusiana na ufanya usajili ndani ya klabu lakini hakuna chochote ambacho alikuwa akikifanya.

Kutokana na sakata hilo, Makele alimalizia kwa kusema Tarimba amekuwa muongo kwa kusema Sanga vibaya, jambo ambalo limeleta mkanganyiko na kupelekea yeye ajiuzulu kwenye nafasi yake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic