SHILOLE AMCHAMBA MUNA “WEWE MWANAMKE UTAPATA TABU SANA”
MSANII wa muziki wa mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amemvaa msanii mwenzake wa Bongo Movies, Rose Alphonce ‘Muna Love’ kwa kuita vyombo vya habari na kuzungumzia kuhusu ugonjwa na kifo cha mwanaye Patrick huku akisisitiza kuwa baba mzazi wa mtoto huyo alikuwa ni Casto wala siyo Peter.
Akifunguka, Shilole amesema halikuwa jambo jema kwa Muna kutoka na kuanza kuzungumzia mambo ambayo tayari yalikwisha siku ya msiba kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar wakatai msiba wa mtoto wake bado mbichi ndiyo kwanza una wiki moja tu.
“Ningekuwamimi ningefunga na kufanya maombi kwa ajili ya mtoto wangu, yani Muna unapata wapi nguvu ya kutoka na kuanza kuongea na vyombo vya habari hata 40 ya mwanao haijaisha? Unapata wapi nguvu ya kushika simu, kumfanyia interview na kumrekodi Steve Nyerere wakati umefiwa?
“Haya mambo yaliisha siku ya mazishi, hakuna chopmbo cha habari wa Instagram yoyote ambayo imekuwa ikiyazungumzia, unataka kumthibitisha mtoto ni wa Casto ili iweje? Hatuhitaji kujua sisi, kwa hiyo ameamua kumdharirisha baba watu Peter? Umeshindwa hata kuficha madhaifu yako au aibu ya wanawake wengine ambao wamezaa nje ya ndoa lakini wanaishi na waume zao?
“Umehangaika na mtoto wako, hadi mtoto akafariki, umeingia leba ukazaa, sielewi, yani roho inaniuma sana, hivi unafuraha gani? Mtoto anauma kuliko kitu chopchote, unaita press conference ili iweje? Itakupa mileage gani? Hakuna mwanamke ambaye amependa hiki, kwa nini kama ungekuwa na tatizo usingeniambia kama mambo mengine ambavyo huwa unafanya, wewe mwanamke utapata tabu sana kwenye hii dunia,” amefunguka Shilole.
0 COMMENTS:
Post a Comment