July 21, 2018




Sasa unaweza kusema ni asilimia 100 kuwa beki Kelvin Yondani, amebaki Yanga.

Yondani ataendelea kuitumikia Yanga baada ya kumalizana na klabu hiyo kupitia Abbas Tarimba.

Tarimba aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga, ndiye aliamua kuchukua jukumu hilo la kumbakiza Yondani baada ya kukutana na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga aliyemuomba.

“Kiukweli, Yondani tumemalizana. Kama yamebaki mambo madogo tu ni kati yangu na yeye. Lakini sasa ni uhakika msimu ujao ataichezea Yanga,” alisema Tarimba alipozungumza na SALEHJEMBE.

Taarifa zinaeleza dau la Sh milioni 60 limetoka ili kumbakiza lakini Tarimba hakutaka kuweka hadharani masuala ya kifedha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic