July 16, 2018


Chelsea ina hamu kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Lazio, Sergej Milinkovic-Savic msimu huu wa joto. Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 23 amehusishwa na uhamisho kwenda Manchester United. (Corriere dello Sport, via Talksport)

Kipa wa Chelsea raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois anasema mkataba aliopewa na the Blues ni "tofuati kuliko mwingine ninaoweza kupata" kwingine. Mchezjai huyo amehusishwana uhamisho kwenda Real Madrid. (Mirror)

Courtois anasema mchezaji mwenzake wa Chelsea Eden Hazard: "Ninako kwenda, Hazard lazima anifuate." Hazard, wa miaka 27, pia amehusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid. (Evening Standard)

Liverpool imewasilisha ombi kutaka kumsajili kipa wa Barelona raia wa Uholanzi Jasper Cillessen, mwenye miaka 29. (Mundo Deportivo, via Talksport)

Mlinzi wa England Luke Shaw, wa miaka 23, yupo tayari kuondoka Manchester United kama ajenti wa bure iwapo hatothibitishwa kuwa chaguo la kwanza la Jose Mourinhokiungo cha beki kushoto msimu huu. (Manchester Evening News)

Everton, Tottenham na Chelsea zote zinamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Boca Juniors Wilmar Barrios, wa miaka 24. (TyC Sport, via HITC)

Mwenyekiti wa Lyon chairman Jean-Michel Aulas anakaribisha kuanzishwa upya jitihada za Liverpool kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Nabil Fekir, wa miaka 24. (Le10 Sport, via Liverpool Echo)

Besiktas wamepewa mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, wa miaka 29, kwa mkopo. (Fanatik, via 90min)


Meneja wa Derby Frank Lampard anakaribia kumsaini winga wa Liverpool Harry Wilson, kwa mkopo. (Mirror)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic